Nyota wa muziki huo nchini, Rose Athuman Muhando.
LILE jinamizi la kupokea
fedha kwa ajili ya kushiriki tamasha la kuimba nyimbo za Injili kisha
kutotokea siku ya tukio linazidi kumwandama nyota wa muziki huo nchini,
Rose Athuman Muhando,
safari hii akidaiwa kumliza tena mtu, Ijumaa Wikienda lina kesi hiyo mkononi.
safari hii akidaiwa kumliza tena mtu, Ijumaa Wikienda lina kesi hiyo mkononi.
Kwa mujibu wa chanzo makini cha ndani, safari hii ameendelea kupokea
fedha kutoka kwa mshirika wake kwenye mambo ya Injili, Alex Msama kwa
makubaliano ya kushiriki Tamasha la Krismasi kwenye Uwanja wa Samora
mjini Iringa lakini siku ya tukio, Ijumaa iliyopita, mwanadada huyo
hakutokea!
Chanzo kilisema: “Hivi jamani mnajua kuwa, Rose Mhando amemliza tena Alex Msama? Amepokea fedha kwa ajili ya kushiriki Tamasha la Krismasi, Iringa lakini pamoja na kupokea fedha hizo ameingia mitini.
“Kusema ukweli huu utapeli wa Rose wa kuchukua fedha za watu halafu hatokei sasa imekuwa too much. Nimesikia habari kwamba ameogopa kutokea uwanjani hapa ambako tamasha lilifanyika kwa kuhofia mimba yake kuonekana maana kwa sasa ni kubwa.”
Bw. Alex Msama.
Baada ya madai hayo, Wikienda lilimvutia ‘waya’, muandaaji wa tamasha
hilo, Msama ambapo alisikiliza kwa muda madai ya mwandishi na mwishowe
alikata simu bila kusema chochote.Rose naye aliposakwa kwa njia ya simu iliita bila kupokelewa ikiwa ni mtindo aliouanzisha siku za karibuni anapotafutwa na waandishi kwa ajili ya ufafanuzi wa habari yake yoyote ile.
Mbali na Msama kudaiwa kulizwa kiasi hicho cha pesa ambacho hakikujulikana ni shilingi ngapi, ikiwa ni mara ya pili ndani ya mwaka mmoja, Rose pia ana madai mengi kutoka kwa watu mbalimbali kwamba amekuwa akipokea pesa kwa makubaliano ya kufanya shoo lakini anaingia mitini kwa kuzima simu au kutopokea akipigiwa.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.

Post a Comment