Vunja ukimya!
Mwanamuziki mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
anayeitumikia Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ ya Bongo, Patchou
Mwamba ‘Tajiri’ ameibuka na kufungukia skendo ya kufumaniwa iliyosambaa
kwa kasi kama moto wa kifuu, Ijumaa Wikienda linakupa mchapo kamili.
Watu mbalimbali mitandaoni, walitumiana picha hiyo huku wakisindikiza na ujumbe wa mtu aliyeiposti awali na kuandika kuwa mwanamuziki huyo amevimba baada ya kufumaniwa na kutembezewa kichapo cha mbwa mwitu.
Wakati Ijumaa Wikienda likiwa katika harakati ya kuchimba ukweli wa jambo hilo (kawaida ya Global Publishers), mwanamuziki huyo alitinga katika ofisi za gazeti hili na kutumia dakika 30 kuanika ukweli kuhusiana na uvumi huo.
“Nimesikitishwa sana na jambo hili. Sijafumaniwa chochote, watu tu wameamua kunichafua. Mimi nina ‘aleji’ na pombe, kuna dawa nilishauriwa niwe nakunywa kila ninapotaka kunywa pombe.
Muonekano wa Patchou Mwamba ‘Tajiri’ baada ya kupata uvimbe usoni.
“Sasa bahati mbaya siku hiyo nikalazimisha kunywa bila kutumia dawa,
uso ndiyo ukavimba namna ile. Sasa nilijipiga picha usoni nikaposti
Instagram na kuwaomba watu ushauri kama wanajua tiba ya ugonjwa wangu
wanisaidie, nikashangaa ghafla watu wakaisambaza picha hiyo na vichwa
vyao tofautitofauti, imenisumbua sana,” alisema Patchou huku uso wake
ukiwa umerudi katika hali yake ya kawaida.Mhariri-Kuna kila sababu ya serikali kupitia Wizara ya Sayansi na Teknolojia kulitazama kwa jicho la tatu suala la watu wanaokurupuka na kuposti picha sizizokuwa na ukweli au ukiukwaji wa maadili maana tatizo hili linazidi kushamiri kwa sasa.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment