Mshereheshaji maarufu Bongo, Glads Chiduo ‘MC Zipompa’.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda wikiendi iliyopita jijini Dar, MC
Zipompa alisema: “Nilimpa muziki akafanyie shughuli yake kwenye Ukumbi
wa Karimjee (Dar), akanilipa laki moja na nusu ikabaki elfu hamsini,
akaniahidi angelipa siku inayofuata lakini kila nikimpigia simu hapokei
na nilipomtumia SMS alijibu yuko Arusha kwenye kikao.”
Staa wa muziki wa Kizazi Kipya, Stara Thomas.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, mwanahabari wetu alimtafuta Stara
ambaye alikiri kudaiwa kiasi hicho cha fedha na kusema kuwa simu yake
iliharibika ndiyo maana alishindwa kuwasiliana na Zipompa ila atamlipa.“Mimi si wa kumtapeli Zipompa hiyo fedha ni ndogo sana kwangu,” alisema Stara.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment