Katika ripoti iliyotolewa na tovuti hiyo, inadaiwa kuwa Rihanna ni mjamzito na walipata taarifa hizo jana huku wakieleza kuwa si tetesi taarifa hizo ni za uhakika asilimia 100.
Mtandao huo uliongea na watu wawili tofauti waliokaribu na staa huyo waliouambia kuwa Rihanna kwa sasa ameelekeza nguvu katika wimbo wake mpya uliopo kwenye albamu yake ambapo ataelekezea
kuhusu ujauzito huo.
Mbali na hilo, inasemekana staa huyo kwa sasa havuti bangi katika studio anazotumia kurekodia wimbo huo jambo ambalo ni ajabu kwa mrembo huyo ambaye anafahamika kwa kupuliza moshi kama dohari.
Inadaiwa pia mrembo huyo kwa sasa ana furaha kubwa kwa kupata ujauzito huo ambao aliugundua hivi karibuni.
Wadau wengi bado wana sintofahamu juu ya nani baba wa mtoto huyo huku wengine wakihisi kuwa huenda muhusika ni Drake.
Mtandao huo umezidi kunyetisha kuwa kuhusu mhusika wa mimba hiyo bado hauna uhakika ni nani ila wao wana uhakika 100% kuwa mnyange huyo ni mjamzito na iwapo kuna mtu anabisha dola 10,000
ziko mezani kwa ajili yake.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment