Staa wa filamu Bongo, Jenipha Kyaka 'Odama'.
MASTAA wa
filamu Bongo, Nisha, Odama na Aunt Ezekiel wameipongeza kampuni ya
Steps Entertainments kwa kitendo chake cha kuagiza mtambo wa kurekodia
filamu kitu ambacho kitawasaidia wasanii kufaidika.“Kitendo cha kurekodia nje ya nchi kilikuwa kinawafanya wasambazaji kuongeza gharama za filamu zetu kwa walaji, kitu ambacho kilikuwa kikiwafanya wanakimbilia kwa wezi wa kazi zetu kwa sababu ya urahisi wa bei, lakini wao kwa kuleta mtambo huo, ina maana filamu zitashuka bei na zikiwa na ubora, ni jambo zuri sana,” alisema Odama akiwa pamoja na wenzake hao.
Staa wa filamu Bongo,Salma Jabu 'Nisha'.
Kampuni hiyo wiki iliyopita ilitangaza kununua mtambo huo ambao
utawezesha filamu zinazotengenezwa nchini kuuzwa kwa bei rahisi lakini
zikiwa na ubora. Aidha, hali hiyo itasaidia pia kudhibiti wizi wa kazi
za wasanii unaofanywa na maharamia kwa kudurufu kazi zao na kuziuza kwa
bei rahisi.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment