Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

KIFO CHA AISHA CHAMUIBUA QUEEN SUZY

 
Mnenguaji wa FM AcademiaSuzan Chubwa ‘Queen Suzy’.

KIFO cha utata cha mnenguaji nyota Bongo, Mwanaisha Mbegu maarufu kama Aisha Madinda, kimemuibua Suzan Chubwa ‘Queen Suzy’ wa FM Academia, aliyewataka wenzake kuwa makini ili kutojiingiza katika utumiaji wa madawa ya kulevya.

Akistorisha na paparazi wetu, Queen Suzy alisema ameumizwa sana na kifo hicho kwani ameacha pengo kubwa kutokana na unenguaji wake mzuri, huku chanzo cha kifo chake kikiwa hakifahamiki sawasawa.
“Nawasihi wanenguaji wenzangu na wanamuziki wote, tusidanganyike kuingia kwenye vishawishi vya matumizi ya madawa ya kulevya, maana mfano Aisha alikuwa mzuri kweli kwenye kazi, lakini alipojiingiza kwenye unga kiwango chake kikashuka sana,” alisema Queen Suzy.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright BONGO HABARI
Back To Top