SIKU chache baada ya kuripotiwa kuwa mjamzito, mimba ya mwigizaji Aunt Ezekiel imezua balaa baada ya mwanamke anayedaiwa kuibiwa bwana na mwigizaji huyo anayefahamika kwa jina la Mwengi kuibuka na kufunguka mazito.
Mwengi ambaye yupo ndani ya bifu zito na
mwigizaji huyo, alizaa na dansa wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’,
Mose Iyobo ‘Moze’ ambaye sasa inasemekana amekolezwa vilivyo na penzi la Aunt.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, siku
chache zilizopita Mwengi alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa
ambapo alitupia picha kibao zikimuonesha akilishana keki na Moze
kuashiria kwamba wana mahaba niue huku akisindikiza na ujumbe huo wa kumtisha Aunt.
Mose Iyobo ‘Moze’ akiwa na familia yake.
“Kazi kwako shangazi hii ndiyo bethidei
halali familia imetimia, toto langu la maana siyo wewe uliyetoa mimba
kibao tutaona na hiyo mimba kama mtoto atazaliwa, haya mume wangu miye
kazana kumchuna pesa huyo shangazi uniletee tutumie atakalia kuchunwa tu yeye shangazi kazi yake si kutoa,” aliandika Mwengi.
Mapaparazi wetu walipomtafuta Aunt ili
kusikia anamzungumziaje Mwengi ambaye amemtupia madongo ya kutosha, simu
yake iliita bila kupokelewa.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment