Kamishna kova ambaye amezungumza na wanahabari muda mfupi uliopita
Kati
ya watuhumiwa 149 waliokamatwa mmoja amegundulika kuwa ni kiongozi
aitwaye ATHUMANI SAIDI miaka 20, Mkazi wa Kigogo na amekiri anaongoza
kundi la watu zaidi ya 15 ambao baadhi yao ni kati ya waliokamatwa.
Imegundulika
pia kwamba vijana hawa wanatumia dawa za kulevya aina ya bangi na
wengine hujichoma sindano na kuwafanya iwe rahisi kujihusisha na matukio
ya uhalifu. Vijana
hao hupenda kushiriki katika ngoma kama Mnanda, Mchiriku, Kigodoro,
Kanga moja nk. ambazo kwa kawaida huchezwa hadi usiku wa manane.
Wakitoka
katika ngoma hizo hujikusanya pamoja na kufanya matukio ya uporaji kwa
mtu wanayekutana naye, kufanya uvunjaji katika majumba na wakati
mwingine wana mtindo wa kugema mafuta ya diesel au petrol katika matanki
ya malori yanayosafirisha mafuta.
Operesheni
kali inafanyika katika maficho ya wahalifu hao ikiwa ni pamoja na
daraja la River side, Kigogo darajani, Manzese, maeneo ya Tandale pamoja
na maeneo mengine ya maficho mkoa wa Kipolisi Temeke.
Tunawasiliana
na Maafisa utamaduni wa Wilaya zote za Mkoa wa D’Salaam kusimamisha
utoaji wa vibali wa ngoma za usiku ambazo hazina tija. Pia Jeshi la Polisi linafuatilia na kuwavizia vijana wanaopora watu wanaotoka katika sherehe za usiku kama vile Harusi na wanaotoka katika mikesha ya Ibada na sehemu zozote zenye mikusanyiko.
Aidha
Jeshi la Polisi wanapambana na vijana wanaowavizia watu katika vituo
vya mabasi pindi wanapotoka alfajiri kwenda katika shughuli zao za kila
siku.
Zipo
taarifa kwamba baadhi ya wazazi wasio waaminifu wamewasafirisha watoto
wao wahalifu katika makundi haya kwenda mikoani ili kukwepa wasinaswe na
msako huu mkali. Hata
hivyo Jeshi la Polisi lina mtandao wa kutosha kati yake na mikoa
mingine na nchi jirani hivyo litawatafuta popote walipo na kuwakamata.
Oparesheni
hii ni endelevu na ya kudumu hadi kero hii ya vibaka itakavyokwisha
kabisa. Baadhi ya majina waliokamatwa ni kama ifuatavyo:-
1. DANIEL PETER @ MALUNDE, miaka 25, mkazi wa Yombo Kigunga
2. MWISHEHE ADAM, miaka 35, mkazi wa Mtoni mashine ya maji
3. MOHAMED SAID, miaka 32, mkazi wa Mtoni
4. JAKAMA ALPHONCE, miaka 23, mkazi wa Mtoni Kilakala
5. HAMADI MDUDU, miaka 25, mkazi wa Mbagala
6. SALUM MUSA, miaka 25, mkazi wa Kiwalani
7. ANTHONY DANIEL, miaka 20, mkazi wa Mashine ya maji
8. FIDELIN ANTHONY, miaka 18, mkazi wa Kigogo
9. HAMZA MAZUMA, miaka 19, mkazi wa Kigogo
10. MGANGA ABEID, miaka 20, mkazi wa Kigogo
11. SAID ABEID, miaka 19, mkazi wa Kigogo
12. SALUM NYENJE, miaka 36, mkazi wa Chamazi
13. DOMINICK PETER miaka 22, Mkazi wa Kigogo
14. KULWA ABEID, miaka 20, mkazi wa Mabibo
15. MUSA IBTRAHIM, Miaka 20, mkazi wa Magomeni
16. HUSSEIN SHABAN, miaka 22, Mkazi wa Magomeni
S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
|
Post a Comment