Frank Kalamu akiombewa kanisani.
Akitoa ushuhuda huo ndani ya Kanisa la The Revelation lililopo
Buza-Kipera Desemba 21 mwaka huu, Frank alidai amepata mateso hayo kwa
muda mrefu huku akizunguka kwa waganga na madaktari wengi bila
mafanikio, mbaya zaidi, kwa kipindi chote hicho ameshindwa kushiriki
tendo la ndoa na mkewe.Akizungumza na waandishi wetu nje ya kanisa, Frank alisema awali alikuwa mzima lakini ghafla alianza kwa kukosa hamu ya kushiriki tendo na mkewe, ingawa alipojaribu kuchepuka, alimudu vyema kazi hiyo.
“Baadaye dalili zilizidi kuongezeka, nikajikuta nikipata maumivu chini ya kitovu na kuanza kutoka damu kila mwezi hasa nikiwa najisaidia haja kubwa, hali hiyo huambatana na kutoka nyama sehemu za haja kubwa.
...Frank Kalamu akizidi kupokea upako.
“Nikawa nikijisaidia kitu kama utumbo unatoka, huku damu zikitoka
pia, siku nyingine japokuwa ‘sikubleed’ lakini nyama hiyo ilitoka na
nikawa nairudishia kwa ndani,” alisema Frank kwa uchungu na kuongeza
kuwa alianza kuhangaika kwa waganga mbalimbali bila msaada wowote.Baada ya kuona anamaliza fedha bila kupata nafuu, Frank aliamua kutafuta huduma ya kiroho ambapo akiwa kanisani hapo, Nabii Yaspi alimwambia kuwa alikuwa amerogwa na mtu aliyemtaja kwa jina la Saidi, ambaye mgonjwa huyo alimtambua kama rafiki yake wa zamani aliyewahi kumhisi kuwa alitembea na mchumba wake.
...akitoa ushuhuda wake.
“Nabii aliponiambia kuwa ni Saidi aliyeniroga, picha ya rafiki yangu
ilikuja kichwani, kila mara alinihisi natembea na mchumba wake. Nadhani
aliniroga kwa sababu hiyo si nyingine,” alisema mtu huyo ambaye pia
alidai kufuatia huduma ya maombezi anayoipata, anaanza kuona dalili za
mabadiliko ya hali yake.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment