Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mwanamama anayekimbiza Uganda, Zarinah Hassan a.k.a Zari au The Boss Lady.
Akizungumza katika mahojiano maalum katika ofisi za gazeti hili,
Bamaga-Mwenge jijini Dar hivi karibuni, bila kupepesa macho au kuuma
maneno baada ya kuulizwa kinagaubaga juu ya ukaribu wake na Zari,
Diamond au Dangote hakutaka kuficha, akaamua kuweka mambo yote
hadharani.MATANGAZO
Alifunguka: “Mimi ni mwanamuziki mkubwa na mwenye heshima, wakati mwingine natakiwa kuwa na akili ya kuwa na uhusiano na watu ambao watakuwa msaada kwangu pia.
“Siwezi kuwa karibu na mtu ambaye hataniongezea kitu chochote kile. Baada ya kujitangaza sana Tanzania, nikahamia Kenya ambapo nilikuwa karibu na mwanadada Avril. Ukaribu wangu kwake, ukanifanya Kenya kutambulika.
“Baada ya kukaa kwa muda, nikataka nitambulike na Uganda pia, unafikiri ningefanya nini? Nikaliteka soko lao kwa kuwa karibu na mrembo Zari.
“Kweli nimefanikiwa na hata siku ya shoo yake (Desemba 18, mwaka huu nchini Uganda), ilikuwa ni balaa kiasi kwamba sikuamini kilichokuwa kimetokea, watu walikuwa nyomi ile mbaya. Mbali na kuwa mwanamuziki mkubwa, bado nahitaji kujitangaza zaidi.”
Zari na Diamondi wakibusiana kimahaba.
MSISIMKOSababu ya pili aliyoitaja ni kwamba Zari ambaye ni mama wa watoto watatu ana msisimko wa aina yake tofauti na ‘mashori’ wengine aliwaowahi kuanguka nao dhambini.
“Hakuna mwanaume anayependa kukaa na msichana asiyekuwa na msisimko wa kimapenzi. Hebu fikiria umekaa na mwanamke mwenye umbo kama la mwanaume, utapata msisimko gani hapo? Lakini mcheki mtoto alivyong’aa, anameremeta, mtoto yupo bomba, ukikaa karibu yake tu utagundua kwamba umekaa na msichana mwenye mvuto ambaye kila wakati atakufanya kuwa bize kumwangalia.”
BIASHARA
Sababu ya tatu aliyoitaja Diamond ni kwamba mwanadada huyo yupo vizuri kibiashara.
“Ninaangalia fedha, ili biashara zangu ziweze kupiga hatua sina budi kukaa karibu na mfanyabiashara mwenzangu (Zari) kwa ajili ya kushauriana biashara ziende vipi.
“Yeye (Zari) ni mkongwe katika biashara, kuwa karibu naye naamini nitajifunza mambo mengi sana.
Amekuwa muwazi kwangu na amenipa mianya mingi ya kufanya biashara, lakini je, nisingekuwa karibu naye, michongo hiyo ningeipata vipi?”
Zari na Diamondi wakiwa kwenye pozi.
UZURISababu ya nne ya kuwa na Zari, Diamond alidai kwamba mwanamama huyo ni mzuri kupita maelezo.
Alifunguka: “Mimi ni mwanamuziki mkubwa, watoto wazuri wananipenda kwa hiyo kama ningefanya uamuzi wa kuwa na mwanamke asiyekuwa mzuri, maneno yangeanza kusikikasikika na isingekuwa poa. Mbali na kuwa mfanyabiashara, kumtumia kama msaada wa kunitangaza, lakini Zari ni mzuri bwana. Ni mwanamke ambaye kwa kumwangalia tu, unaweza kusema kwamba haujawahi kukutana na mwanamke mzuri kama yeye.
ANAJITAMBUA
Sababu ya mwisho aliyoianika Diamond ni kwamba Zari yupo vizuri kichwani kwa maana ya kujitambua tofauti na wanawake wote aliowahi kutembea nao.
Mwanadada mwenye mvuto Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’.
“Nimekuwa na wanawake tofautitofauti lakini kwa Zari, ni mwanamke
mwenye hekima na anajitambua sana. Si mzungumzaji kivile na huwa
anapenda kufanya vitendo kuliko maneno.“Anajua ni kipi anatakiwa kufanya na akili yake ameielekezea kwenye fedha zaidi. Hapendi masihara na fedha, anapenda kujitoa na ni mchakarikaji sana. Nampenda mwanamke wa hivyo kwa kuamini kwamba atanifanya nijitume zaidi.”
AWACHAMBUA JOKATE, WEMA NA PENNY
Diamond alipoulizwa juu ya kasoro za warembo wakali Bongo aliowahi kutoka nao wakiwemo mrembo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, Wema na mtangazaji wa Radio E-FM, Penniel Mungilwa ‘Penny’, aliwachambua mmoja baada ya mwingine na kuhitimisha kuwa ni wazuri lakini hawamfikii Zari.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
UTAMBULISHO KESHO DAR LIVEMbali na kuziweka wazi sifa za Zari, jamaa huyo alidai kwamba atamtambulisha rasmi kwa Wabongo kesho usiku kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Burudani wa Dar Live, Mbagala jijini Dar atakapokuwa anaangusha burudani ya kibabe katika Tamasha la Wafalme akiwa na mfalme mwenzake, Mzee Yusuf na wakali wengine kibao kwa kiingilio cha shilingi 10,000/= kwa kawaida na shilingi 20,000/= kwa V.I.P.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment