Kijana
mmoja nchini zimbabwe katika kijiji cha pote amekimbia kijiji hicho
baada ya kujikuta katika matatizo makubwa kufuatia kumtia mimba mama
yake mzazi kwa mara ya pili.
Ikumbukwe
hapo nyuma kijana huyo aliwahi kutenda kitendo hicho ambapo wana kijiji
walimsihi kutorudia tena kitendo hicho baada ya kijana huyo kumshawishi
mama yake na kuitoa mimba hiyo.
Simon Matsvara na mama yake Ethel Vhangare aliamua kuondoka baada ya waumini wa kanisa lao kugundua kuwa mimba hiyo ni batili.
Miaka minne iliyopita, wawili hao waliripotiwa na kutozwa faini na viongozi wa kijiji kwa kosa la kutoa mimba.
Chifu
wa kijiji, Chinamhora alisema kuwa jamii ilikasirishwa na kitendo hicho
na kwamba yeye aliamua kuwatuma wafanyakazi wake kuwatafuta wawili hao
waliokuwa wameamua kuishi kama mume na mke.
“Tunaenda
kuwatafuta mpaka tuwapate na wakisha patikana ni lazima wapewe adhabu
kali ili iwe fundisho kwa watu wengine wanoa jihusisha na vitendo kama
hivyo ambavyo havikubaliki katika jamii”Alisema chifu huyo.
Imeripotiwa
kuwa wawili hao walianza mahusiano yao tangu mwaka 2008 wakati Matsvara
alipopewa jukumu la kumuuguza baba yake mzazi mzee Agripah,ambae baadae
alikufa.
Mama huyo alipata mimba mara ya kwanza, wawili hao walitozwa faini na kuambiwa uhusiano wao ukomee hapo wasije wakarudia tena.
Habari
ya mimba ya pili ziligundulika baada ya mama huyo kuanza kuwakwepa
waumini wa kanisa lake walipokuwa wakimtembelea nyumbani kwake.Baada ya
uchunguzi ndipo walipogundua kuwa mama huyo ni mjamzito wa miezi 5 na
ujauzito huo kapewa na mwanae.
“Wawili hao wameamua kukimbia kijiji chao baada ya kugundulika wamejihusisha na kitendo hicho.”
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment