Ukifika
nje ya geti la Kituo cha Masanga tangu mwezi huu wa 12 ulipoanza
utakutana na huu ujumbe ''HAKATWI MTU HAPA'' hiki ni kituo cha kuzuia
ukeketaji (TFGM) ambacho kinatoa mafunzo ya ukeketaji mbadala na tohara
salama... kwa sasa kuna watoto zaidi ya 600 ambao wamekimbilia hapa ili
wasikeketwe tangu msimu huu ulipoanza mwezi wa 12/2014...
Mwezi wa 12 ni mwezi wa kufanya tohara mkoani Mara ambapo watoto wengi huwa wamefunga shule na hivyo kupelekea watoto wa kike hukeketwa...
Mwezi wa 12 ni mwezi wa kufanya tohara mkoani Mara ambapo watoto wengi huwa wamefunga shule na hivyo kupelekea watoto wa kike hukeketwa...
Pata mwonekano wa Kituo cha Masanga, ambacho kipo katika kijiji cha Masanga Wilaya ya Tarime Mkoa wa Mara...
Kituo
hiki cha Masanga kinategemea sana maji ya mvua, na mvua hazijanyesha
siku za karubuni, jmosi iliyopita waliletewa maji na Mkuu wa Wilaya ya
Tarime.... kwa hiyo wanahitaji msaada wa haraka sana sana...
Mabango haya yamebeba ujumbe tofautitofauti kwa lengo la kuifikishia jamii kilio chao kutokana na hii mila yao ya Ukeketaji...
Niliwatia
moyo kwamba wakati mwingine inabidi wasisubiri kufanyiwa MAAMUZI hasa
yale maamuzi yenye madhara kama hii mila ya Ukeketaji...
Watoto waliokimbilia kituo cha Masanga kujiokoa na kisu cha msumu huu wa Ukeketaji mkoani Mara...
Watoto
zaidi ya 600 wakitoa sauti zao kupinga kukeketwa mwezi huu wa 12/2014..
wanahitaji msaada wa dharura kama Maji, chakula, pedi, n.k
Watoto
wakitoa sauti zao nje ya kituo cha Masanga kuieleza jamii ya Tanzania
na Dunia nzima juu ya Mila yao ya Ukeketaji ambayo inawakandamiza
wasichana kwa kiasi kikubwa...
Nimeona
ni busara kuwaomba Umma tushirikiane kuwasaidia watoto hawa hasa
kipindi hiki kigumu ambacho wamekimbia kukeketwa wakingojea msimu uishe
mwezi huu wa 12 warudi makwao wakaendelee na shule... yaani hawana hata
maji! kama ujuavyo maji ni muhimu sana kwa binadamu, na huwa wanategemea
maji ya mvua!!! sasa mvua hazijanyesha hivi karibuni... pia hawana
chakula, pedi, nguo, viatu, kama una maswali zaidi unaweza kumuuliza
mkuu wa kituo hicho Sister Germana... Lakini chondechonde nakuomba
tuwasaidie wako kwenye hali mbaya...
Msimu wa Ukeketaji ukiendelea, Watoto hawa wametoka kukeketwa.... baadhi ya watoto wamekimbilia kituo cha Masanga...
Msimu
wa ukeketaji ndo umepamba moto Trime...wakati watoto zaidi ya 600
wakitorokea Masanga, huku wengine wanaendelea na Tamasha la Ukeketaji
kama kawaida.... Kikubwa ni kutoa elimu kwa jamii juu ya mila hii
inayomkandamiza mtoto wa kike... Lakini kwa sasa tuwaokoe watoto wetu na
hali iliyopo hivi sasa....
Nilipata wasaa wakuongea na Wazee wa Koo 13 Tarime juu ya hii mila ya Ukeketaji na jinsi hali halisi ilivyo...
Wawakilishi
wa Wazee wa Mila Koo 13 Tarime.... mengi utayasikia kwenye kipindi cha
@wanawakelive ila kwa sasa MSAADA WA HARAKA UNAHITAJIKA....
Huyu
ndo Mkuu wa kituo kile cha Masanga chenye wasichana zaidi ya 600
waliokimbia kukeketwa, anaitwa Sister Germana.... Namba zake zipo kwenye
bana lenye maandishi ya kuomba msaada wa dharura....
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI
Post a Comment