NATISHA! Uhaba mkubwa wa madawa, ongezeko la ada ya kitanda na chakula katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, umesababisha watu wengi kupoteza maisha kufuatia wagonjwa kukosa huduma na hivyo kurejea majumbani mwao.
Katika wodi ya wagonjwa wa moyo,
walilalamikia bei kubwa ya matibabu inayowafanya wasio na uwezo na wasio
na ndugu kuishi kwa kubahatisha. “Hali ni mbaya sana hapa, jana
nimeshuhudia wagonjwa wenzetu wawili wanapoteza maisha kwa sababu
hawahudumiwa tokea majuzi kwa vile hakuna dawa, na tunasikia hata huko
katika mawodi mengine hali ni ya hatari kabisa,” alisema mgonjwa mmoja
aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Hali ilikuwa hivyo pia katika majengo
mengine, likiwemo lile la watoto, ambako wagonjwa walionekana kuwa ni
wengi kuliko wauguzi, kwani wakati kwa wastani muuguzi mmoja anapaswa
kuhudumia wagonjwa kati ya 5-8, hapo muuguzi mmoja alijikuta akihudumia
hadi wagonjwa 60.
Hata duka la dawa lililo chini ya hospitali hiyo, nalo lilionekana kama urembo tu, kwani kila aliyeandikiwa, alilazimika kutoka nje kwenye maduka binafsi.
Hata duka la dawa lililo chini ya hospitali hiyo, nalo lilionekana kama urembo tu, kwani kila aliyeandikiwa, alilazimika kutoka nje kwenye maduka binafsi.
Kwa wagonjwa waliotakiwa kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu zaidi, waliambiwa kurejea majumbani hadi hapo watakapoitwa kwa simu baada ya serikali kupata fedha.
Huduma ya maji pia ni tatizo lingine
linalowakabili wagonjwa waliopo hospitalini hapo, kwani kwa wasiokuwa na
uwezo wa kununua maji ya chupa, inawawia vigumu kuyapata kutoka
Dawasco.
Vinginevyo wanapaswa kuyatumia yanayotoka katika kisima kilichopo hospitalini hapo, ambacho hata hivyo maji yake yanaelezwa kuwa na chumvi.
Vinginevyo wanapaswa kuyatumia yanayotoka katika kisima kilichopo hospitalini hapo, ambacho hata hivyo maji yake yanaelezwa kuwa na chumvi.
Afisa uhusiano mkuu wa Hospitali hiyo,
Emaniel Eligalesha alisema matatizo yote yanayohusu hospitali hiyo
yatashughulikiwa muda mfupi ujao.
chanzo; GPL.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment