Mwanamume huyo alionekana akotoka nje ya nyumba yake huku damu ikimwagika kutoka kwa sehemu zake nyeti kufuatia upasuaji aliojifanyia mwenyewe. Msanii huyo mwenye umri wa miaka 38 ambaye nyota yake ilikuwa inang’ara sana alikimbizwa hospitalini kwa huduma ya dharura kwa hofu ya hali yake kuwa mbaya .
Madaktari walijaribu kumshona lakini hawakufanikiwa katika juhudi zao za kumrejeshea mwanamume huyo uume wake. Afisa mmoja hospitalini ambako muigizaji huyo alipokea matibabu alisema alikuwa na bahati sana kuponea kwani alivuja damu nyingi na kwamba angepoteza muda kidogo tu angefariki. Kwa mujibu wa jarida la Mirror, jirani ya Evgniv Sapaev, Arkhip Tikhonov mwenye umri wa miaka 57 alishtuka sana alipombishia mlango na kujionea hali yake akiwa tayari ameanza kudhoofika kwani alikuwa amepoteza damu nyingi sana. “Alionekana akitisha sana akiwa na damu mikononi mwake huku akishika sehemu yake ya uuma ambayo alikuwa ameikata.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment