Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Novemba
6, mwaka huu, majira ya saa 12 jioni, baada ya watoto wenzake aliokuwa
akicheza nao kudai kuwa Nuru alichukuliwa na mtu aliyekuwa amevalia
mavazi ya Kininja na kutokomea naye.
Baadhi ya mashuhuda waliokuwa eneo la
tukio, walisema mwili wa mtoto huyo ulikutwa ukiwa hauna sehemu za siri,
matiti, nyama ya kisogoni na makalio kukatwa na kuzibwa na gundi hali
iliyoashiria ushirikina.
BABA MZAZI PICHANI ASIMULIA ILIVYOKUWA
“Nakumbuka siku ya kutoweka kwake, nilikua kazini nikapigiwa simu saa 12.45 jioni na kuelezwa Nuru ametekwa na mtu aliyevaa kininja, aliyemrubuni kwenda kumnunulia biskuti. “Nilielezwa kwamba muda mfupi baada ya kutoweka, watoto wenzake walipatwa na hofu na kumwambia mama yake kwamba kuna mtu kaondoka na marehemu hali iliyomfanya kuinuka na kuanza kufuatilia bila mafanikio.

“Niliungana na mke wangu pamoja na ndugu
wengine kumtafuta hadi asubuhi bila mafanikio, nikiwa nipo maeneo ya
Chamazi saa 2 asubuhi nilipigiwa simu na kuambiwa mwili wa mwanangu
umepatikana maeneo ya lwa Mkandawile ukiwa umeharibika, nilienda na
kukuta kuwa ni yeye.
“Tulitoa taarifa polisi ambao walifika eneo
la tukio na kuuchukua mwili hadi Hospitali ya Amana na muda mfupi baada
ya kufanyiwa uchunguzi na madaktari tuliuchukua na kuuzika makaburi
yaliyopo maeneo ya ninakoishi,” alisema.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment