MTOTO mmoja wa miaka 9 (jina linahifadhiwa) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Manda iliyopo Kijiji cha Mtimbira, wilayani Ulanga, Morogoro wiki iliyopita usiku wa manane anadaiwa kukutwa darasani akiwa na hirizi kubwa kiunoni.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo lililoshuhudiwa pia na mwandishi wetu, lilijiri Alhamisi iliyopita ambapo mara baada ya kuonekana darasani humo, baadhi ya wananchi walianza kumpa kichapo wakidai kuwa yeye ni mwanga.
Dogo huyo alinusurika kifo kutoka kwa
wananchi hao wa Kigurunyembe waliokuwa na hasira kali baada ya mmoja wa
walimu kuwatuliza na kufanikiwa kumuokoa mwanafunzi huyo na kwenda
kumficha kwenye ofisi ya walimu ya shule hiyo.
Akihojiwa na Uwazi mwalimu huyo aliyejitambulishwa kwa jina la Zuhura Khatibu alikuwa na haya ya kusema:
“ Wiki hii mimi ni mwalimu wa zamu nilipofika shuleni nikawashuhudiwa wananchi wakimshushia kichapo mtoto huyo, kama mzazi niliumia sana nikawauliza kwa nini wanampiga wakadai eti ni mwanga ameanguka hapa shule usiku, sisi tulipigwa butwaa. Nilimuoka na kumficha ofisini,” alisema Zuhura.
“ Wiki hii mimi ni mwalimu wa zamu nilipofika shuleni nikawashuhudiwa wananchi wakimshushia kichapo mtoto huyo, kama mzazi niliumia sana nikawauliza kwa nini wanampiga wakadai eti ni mwanga ameanguka hapa shule usiku, sisi tulipigwa butwaa. Nilimuoka na kumficha ofisini,” alisema Zuhura.
Alipoulizwa alikuwa anaelekea wapi usiku
huo, alidai walikuwa wakienda Kihonda kwa baba yake anayefanya biashara
ya mbogamboga. Alipopekuliwa alikutwa na hirizi kubwa yenye rangi
nyekundu kwenye mkanda wa suruali yake, alipoulizwa ilikuwa ya nini
alisema alifungwa ili kumlinda.
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi wa Dawati la Jinsia na Watoto, Sophia Ngosso alimpokea mtoto huyo na kufungua taarifa kwenye kitabu cha kumbukumbu cha polisi jalada namba MOR/RB/12659/014.
Baadaye iligundulika kuwa mtoto huyo
alikuwa anatafutwa na baba yake aitwaye Clarence Kandira ambaye alifika
pale polisi baada ya kupigiwa simu ambapo alimtambua mwanaye na kuangua
kilio na kusema:
Alipoulizwa kwa nini amemfunga hirizi, Kandira alidai kuwa haikuwa hirizi bali ni alama yake inayomsaidia kuonekana kirahisi anapopotea. Afande Sophia alimsainisha Kandira na kumkabidhi mtoto wake akaondoka naye.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment