Hatari! Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 8 (jina linahifadhiwa kimaadili), mkazi wa Kihonda mjini hapa anayesoma darasa la kwanza kwenye Shule ya Msingi Noto Sosario, anadaiwa kutumika kumwiba mtoto mwenzake kisha kukamatwa na kunusurika kuuawa na wananchi wenye hasira zaidi ya 300.
Tukio hilo la kushangaza lililonaswa na
Ijumaa Wikienda lilijiri wiki iliyopita mishale ya saa 8:00 mchana
maeneo ya Majengo Mapya, Kata ya Kihonda jirani na nyumbani kwa
aliyekuwa staa wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, marehemu Alberth Keneth
Mangweha ‘Ngwea’.
Akizungumza na mwanahabari wetu, mmoja wa
mashuhuda wa tukio hilo, Mama Seleman alisema: “Mtoto huyu alikamatwa
kwa jirani yangu, Asha Tembo akidaiwa kutaka kuiba mtoto wa mama huyo
kwa njia za kichawi hivyo mama huyo aliamua kupiga kelele na kumuitia
mwizi.
“Baada ya kuona watu wanazidi, nikaamua kumwokoa na kumficha ndani kwangu.
“Nikiwa ndani umati wa watu ulitishia kuchoma nyumba yangu lakini nilifunga milango kisha nikawaita polisi wakaja kumuokoa mtoto huyo.”
“Nikiwa ndani umati wa watu ulitishia kuchoma nyumba yangu lakini nilifunga milango kisha nikawaita polisi wakaja kumuokoa mtoto huyo.”
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI
Post a Comment