
Ulozi!
 Chipukizi sinema za Kibongo, Fatuma Ayubu ‘Fetty’ amenaswa makaburini 
akiwanga katika kile kinachodaiwa kuwa ni kutekeleza masharti ya 
‘sangoma’ ili ajipatie umaarufu na kuwafikia mastaa kama Wema Isaac 
Sepetu, Jacqueline Wolper Massawe na Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Chipukizi sinema za Kibongo, Fatuma Ayubu ‘Fetty’. 
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tukio hilo lilijiri wikiendi iliyopita 
kwenye Makaburi ya Ufi yaliyopo maeneo ya Ubungo-Kisiwani jijini Dar, 
mishale ya saa nne usiku.
Fatuma Ayubu ‘Fetty’ akiandaa mazingira. 
...Akiendelea kuandaa. 
...Akivunja nazi kaburini. 
Habari zilidai kwamba msanii huyo alifumwa akivunja nazi na kuzungumza maneno yasiyoeleweka.
Awali,
 ilidaiwa kwamba, Fetty ambaye anaonekana kwenye Filamu ya House of 
Death akiwa na mwigizaji Kulwa Kikumba ’Dude’ alitinga kwenye makaburi 
hayo akiwa ameshika kimfuko huku akiangaza huku na huku kisha akatoa 
nazi na kuivunja huku akinuiza maneno bila kujua kuna mtu alikuwa 
akimpiga picha.
...Akiendelea kufanya yake. 
Ijumaa Wikienda lilipomtafuta Fetty na kumuuliza juu ya madai hayo, 
alianza kujikanyaga kabla ya kufunguka kuwa hapendi mambo ya kishirikina
 ila alilazimika kufanya hivyo kutokana na masharti aliyopewa na mganga 
wake kutokana na matatizo yake ya kimaisha yanayomsumbua pamoja na ndoto
 yake ya kuwa msanii mkubwa.
Vipande vya nazi vikiwa kaburini baada ya kuvunjwa na Chipukizi sinema za Kibongo, Fatuma Ayubu ‘Fetty’. 
Source; GPL.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI. 
Get Free Email Updates to your Inbox!
 
 
Post a Comment