Klabu za Arsenal , Liverpool na Real Madrid ziko kwenye vita kali ya kuwania kumsajili kipa wa Chelsea Petr Cech .
Chelsea inaalzimika kumuuza kipa huyo kwa kuwa hana nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza baada ya kurudi kwa kipa Mbelgiji Thibaut Courtois .
Hadi sasa Chelsea haijapoteza mchezo wowote msimu huu huku Thibaut akicheza kwenye mechi karibu zote hali inayomfanya Cech kulazimika kutafuta mahali kwingine ambako atakuwa chaguo la kwanza .
Cech ameidakika Chelsea kwa mafanikio makubwa kwa muda wa miaka 11 tangu aliposajiliwa kwa mara ya kwanza akitokea Rennes ya Ufaransa .
Cech analazimika kuondoka baada ya kupokonywa nafasi kwneye kikosi cha kwanza.
Akijibu maswali ya waandishi wa habari kocha wa Chelsea Jose Mourinho alikanusha taarifa kuhusu Cech kuwa mbioni kuhama ambapo alisema kuwa hajawahi kupata taarifa yoyote kama hiyo .
Thibaut Courtois ndio kipa namba moja kwenye ikosi cha Chelsea.
Hadi sasa inafahamika kuwa Arsenal ndio iko kwenye nafasi ya juu kumsajili Cech kwa thamani ya puandi milioni 7 lakini kumekuwa na ishara toka kwa klabu za Ac Milan , As Roma , Real Madrid na Liverpool za kutaka kumsajili Cech .
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment