UPEPO mbaya unaendelea
kuvuma ndani ya Klabu ya Bongo Movie Unity! Safari hii umewakumba mastaa
wakubwa klabuni hapo, Devotha Mbaga, Aunt Ezekiel na Jennifer Kyaka
‘Odama’ ambao wanadaiwa kutimuliwa kundini kwa sababu ya kujiweka karibu
na mwenyekiti wa klabu hiyo aliyejiuzulu, Steven Mengere ‘Steve
Nyerere’.
Mwanadada anaye tamba katika tasnia ya filamu bongo, Aunt Ezekiel
Kwa mujibu wa chanzo makini kilichozama katika kikao kilichofanyika
juzikati, uongozi ambao ulibaki madarakani kundini baada ya Steve
kujiuzulu, ulifanya tathmini upya ya memba waliobaki kisha kuwachuja
hadi kubaki na wasanii 20 pekee wenye sifa.
“Wamewaengua baadhi ya wasanii ambao
wameona hawana sifa ya kubaki kundini, miongoni mwao ni Devotha, Aunt na
Odama. Wamesema wanahitaji mastaa wenye msimamo siyo kujipendekeza
upande wa Steve, siku si nyingi watayaanika majina ya wenye sifa za
kubaki kundini,” kilisema chanzo hicho.
Staa wa filamu bongo Devota Mbaga.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ‘ubuyu’ kuwa, wasanii walioenguliwa ni
wanachama hai lakini si wanachama wenye msimamo na baadhi yao wameonesha
udhaifu wa kuwa karibu na Steve Nyerere ambaye sasa anafanya harakati
zake peke yake.
Baada ya habari hizo kutua katika rada ya
Ijumaa, mapaparazi wetu waliwaendea hewani mastaa hao wakubwa waliodaiwa
kufukuzwa, mambo yalikuwa hivi:
Mkali wa filamu Bongo, Jennifer Kyaka 'Odama'.
Devotha: Mimi ndiyo kwanza nakusikia wewe siku zote nipo nyumbani
sijui hata habari za kikao hicho na sielewi wameniengua vipi wakati mimi
ni mwanachama hai na ni miongoni mwa waanzilishi toka tulipokuwa watu
saba, lakini kama wameamua hivyo sawa kwani siyo kwamba ukitoka ndiyo
mwisho wa maisha.Odama: Hakuna kitu kama hicho, wanaoenguliwa ni viongozi siyo wanachama, watanienguaje bila kunipa taarifa? Kwanza ndiyo nasikia sijui chochote ndiyo napata taarifa kutoka kwako.
Kwa upande wa Aunt Ezekiel, simu yake iliita bila kupokelewa.
Post a Comment