Kama ilivyo ada naye anajibu maswali 10
yahusuyo maisha yake binafsi na kisanii ambayo paparazi wetu Hamida
Hassan alimbana na aliyajibu kama ifuatavyo;
Mkali katika tasnia ya filamu bongo, Halima Yahaya 'Davina'.
Ijumaa: Najua una dada wa kazi, unapokuwa nyumbani huwa unafanya nini?Davina: Licha ya kuwa na dada wa kazi, nikiwa nyumbani si mtu wa kukaa tu, napenda kufanya usafi wa nyumba yangu, kupika na kucheza na mtoto.
Ijumaa: Je, ni chakula gani unachopendelea kumpikia mumeo?
Davina: Kiukweli mume wangu anapenda sana makaroni na nyama ya kusaga, ili kumfanya awe na furaha huwa nampikia chakula hicho.
Ijumaa: Ni sehemu gani ya mwili wako unayoipenda zaidi?
Davina: Sibagui, kila sehemu ya mwili wangu naipenda na namshukuru Mungu kwa kuniumba hivi nilivyo.
Ijumaa: Uwapo chumbani na mumeo, nguo gani ambazo unapendelea kumvalia?
Davina: Hahaha, niwapo eneo hilo navaa nguo lainiii na vipensi ndiyo usiseme!
Ijumaa: Kiufupi wewe ni mrembo, unamvutia kila mwanaume, unajilinda vipi na vishawishi vya wanaume wakware?
Davina: Namshukuru Mungu kwa kunipa ndoa kwani ndiyo inanifanya naweza kuepuka vishawishi. Najiheshimu na kuiheshimu ndoa yangu.
Ijumaa: Ikitokea umebaini mumeo kakusaliti utachukua uamuzi gani?
Davina: Kwanza ni kitu ambacho sikitarajii kabisa kutokana na mapenzi anayonionesha na uaminifu alionao.
Ijumaa: Ikitokea umebaini mumeo kakusaliti utachukua uamuzi gani?
Davina: Kwanza ni kitu ambacho sikitarajii kabisa kutokana na mapenzi anayonionesha na uaminifu alionao.
Davina akipozi.
Ijumaa: Kwa nini hivi sasa umekuwa ukiigiza sana sehemu ya mama tofauti na ilivyokuwa huko nyuma?Davina: Unajua hivi sasa mimi ni mama, kwahiyo ninapoigiza nafasi hiyo huwa navaa uhusika ipasavyo. Hata hivyo, nafasi nyingine pia huwa nafanya vizuri.
Ijumaa: Umejaaliwa kupata mtoto mmoja, je una mpango wa kuongeza mwingine na je unatarajia kuwa na familia ya watoto wangapi?
Davina: Siwezi kusema nahitaji familia ya watoto wangapi ila Mungu atakaonijaalia. Kwa sasa sina mpango wa kuongeza mwingine mpaka baadaye sana.
Ijumaa: Wewe umeolewa, unawazungumziaje wasanii wenzako ambao wana watu wao lakini wanachepuka tena wakati mwingine bila kificho?
Davina: Nihimize wasanii kujiheshimu na kuziheshimu ndoa zao, kama wana wapenzi basi watulie. Hii kurukaruka hasa katika ulimwengu wa sasa ni kujitafutia matatizo katika siku zijazo.
Ijumaa: Unayazungumziaje haya mabifu ndani ya Bongo Muvi?
Davina: Unajua maendeleo hayawezi kupatikana kwenye sanaa kama hatutakuwa kitu kimoja. Mabifu si kitu kizuri, mimi nasema tuna kila sababu ya kuondoa tofauti zetu.
Post a Comment