Staa
wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ akilia kwa uchungu
katika mazishi ya msanii mwenzake katika tasnia ya filamu, Recho Haule.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Sinza – Palestina kulipokuwa na
msiba wa Recho, Johari alisema Recho alikuwa na kiu ya kufika mbali na
hakuchoka kuomba ushauri na kuufanyia kazi.
Recho haule (kushoto) akiwa na mke wa Mtitu enzi za uhai wake.
“Amefanya kazi na RJ Company muda mrefu, baadaye akaamua kuanza
kufanya kazi zake akishirikiana na Saguda. Mwanzo ulikuwa mzuri sana,
alikuwa akitaka kitu chake anaweza kupiga simu hadi usiku kuomba
ushauri. Kwa kweli sitamsahau, nitamlilia milele,” alisema Johari.
Post a Comment