HABARI ya mjini ni kwamba, lile penzi linalonadiwa la Mbongo-Fleva, Omary Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ na mwigizaji Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ limejaa magumashi, ikidaiwa kuwa jamaa huyo kawekwa kama boya tu, nyuma yake kuna kigogo mzito serikalini ndiye anayekula vinono, Risasi Jumamosi limetonywa.
“Kutokana na unyeti wa kazi yake, jamaa hataki kujitokeza ‘front’ ndiyo maana ameamua kumtumia Dimpoz kama kanyaboya huku yeye akiendelea kula vyake,” kilisema chanzo hicho.Kikizidi kumwaga ubuyu, chanzo hicho kilidai kigogo huyo ndiye anayedhamini safari zote za Wema na Dimpoz nje ya nchi ikiwemo ile ya juzikati nchini Marekani ambayo ilibuma.
“Jamaa ana pesa chafu, amemnunulia Wema viwanja viwili kimoja kipo Tabata na kingine Kigamboni, Dar, ndiye anayemwezesha Wema katika shughuli zake za kila siku.“Kigogo huyo ndiye chanzo cha Wema kummwaga Diamond, alimpotezea kwa sababu ya maslahi zaidi, hata kwenye bethidei ya Wema mwaka jana, kigogo huyo ndiye aliyegharamia vitu kibao hadi kusababisha Diamond ahoji,” kilisema chanzo chetu.
“Ujue sasa hivi mimi sitaki malumbano na mtu, najua kila mtu siku hizi anaongea kila anachojisikia, naomba niachwe na maisha yangu, unayoyasema hayana maana, wanasema kwa sababu hakuna anayemjua mpenzi wangu wa sasa sina muda wa kubishana.”
Hivi karibuni, wakiwa Sauz, Wema na Dimpoz, picha zao wakiwa kimahaba zilivuja mitandaoni hivyo kuibuka gumzo kuwa huenda kwa sasa nao wanatoka.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI
Post a Comment