Mwanadada anayeendesha maisha yake kwa kuuza sura kwenye filamu za
Kibongo, Kajala Masanja amefunguka kuwa ni muda muafaka wa kufanya
mishemishe za kumtafuta mtoto mwingine kwani yule wa kwanza, Paula
ameshakua.
Kajala Masanja akiwa na mwanaye Paula.
Akizungumzia mipango yake kwa sasa hasa kwenye suala la kuongeza
mtoto, Kajala alisema umri unazidi kuyoyoma na Paula anazidi kuwa mkubwa
hivyo ni vyema akamtafutia mdogo wake fasta kabla ya kuamua kutulia.
“Kwa kweli nahitaji kumpata mdogo wake Paula haraka, umri unazidi
kusonga mbele, siyo nakuja kuzaa tena Paula kishakuwa mdada mkubwa,
itakuwa aibu,” alisema Kajala.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment