Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

YAYA TOURE ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRIKA MARA 4 MFULULIZO

Yaya Toure.
KIUNGO wa Manchester City, Yaya Toure amekuwa mchezaji wa kwanza kushinda tuzo ya CAF ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa mara ya nne mfululizo.
Toure, 31, alitajwa kuwania tuzo hiyo baada ya kutoa mchango mkubwa kwa Manchester City kushinda Ligi Kuu ya England na kunyakua Kombe la Ligi.
Pia aliisaidia Ivory Coast kufuzu kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika 2015.
Toure alipambana na mshambuliaji kutoka Gabon Pierre-Emerick Aubameyang na kipa wa Nigeria Vincent Enyeama.
Toure pia alitajwa kuwania tuzo ya Ballon D'Or Oktoba mwaka 2014.
Mshambuliaji wa Everton Samuel Eto'o ni mchezaji mwingine pekee kuwahi kushinda tuzo ya CAF ya mchezaji bora Afrika mara nne, ingawa sio mfululizo.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright BONGO HABARI
Back To Top