Wafanyabiashara wa mifugoa mjini Bukoba wamegoma kuchinja mifugo yao na
kutofungua mabucha wakilalamikia kuamrishwa na serikali kupunguza bei ya
nyama kutoka shilingi 5,000 hadi 4,000 kwa kilo.
Wakiongea
katika machinjio ya Rwamishenye mjini Bukoba wafanyabiashara hao
wamesema wamegoma kuchinja mifugo hiyo na kutofungua mabucha kabisa
kutokana na barua waliyopewa kutoka kwa mkurugenzi wa halmashauri ya
manispaa ya Bukoba, ya kuwataka kupunguza bei ya nyama hali ambayo
imepelekea wafanyabiashara kususia barua hiyo na kugoma kuchinja mifugoa
yao.
Kwa upande wake mwenyekiti wa wafanyabiashara hao Haji Yatubu Musa amesema wao hawawezi kuchinja mifugo hiyo kutokana na changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika kununua mifugo hiyo na kuisafirisha ambapo amezitaka mamlaka husika kuangalia upya suala hilo na kulitafutia ufumbuzi.
Mpekuzi ilimtafuta mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba Chibunu Lukiku ambapo alidai kwamba leo siyo siku ya kazi na kuwa yeye siyo mchinjaji wa mifugo hiyo.
Akizungumza kwa njia ya simu mkuu wa wilaya ya Bukoba Sporah Pangani amesema ni kweli wafanyabiashara hao walipelekewa barua ya kupunguza bei ya nyama kwa kuwa walipandisha bei kiholela bila kibali kutoka kwenye mamlaka husika hali ambayo imepelekea usumbufu kwa wananchi wa mkoa huo.

USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment