Mwimbaji nyota wa muziki wa Injili nchini, Rose Muhando.
MWIMBAJI nyota wa muziki wa Injili nchini, Rose
Muhando ambaye hivi karibuni alikanwa na aliyewahi kuwa meneja wake wa
muda mrefu, Alex Msama, anadaiwa kuweweseka asijue la kufanya kufuatia
hatua hiyo.
Akizungumza kutoka Dodoma yalipo makazi ya mwimbaji huyo, mmoja wa
watu wake wa karibu aliyeomba hifadhi ya jina lake, alisema hatua ya
Msama kutangaza kutofanya naye kazi, limekuwa pigo kwake kwani ndiye
aliyekuwa kiongozi na mwokozi wake wa mambo mengi ya kikazi na binafsi.
Meneja wa Rose Mhando, Alex Msama.
“Anaweweseka kwa kweli na hajui la kufanya, Msama ndiye alikuwa
msaada wake mkubwa kwa kila kitu kuhusiana na muziki japo kwa sasa
amekuwa hataki hata kumsikia Rose,” alisema mtu huyo.Rose alipigiwa kutaka kusikia kutoka kwake, lakini simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi ulionyeshwa kupokelewa bila majibu. Msama alipoulizwa kuhusu kilio cha msanii huyo alisema yeye ameshatoa msimamo wake na unaeleweka.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment