Neno “piga” lina maana ya “fanya kitendo cha kukutanisha vitu
kwa nguvu, fumua, ezeka, zaba, shambulia, chapa na tandika” kwa mujibu
wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu, Oxford, lakini kwa Waziri Mkuu Mizengo
Pinda neno “wapigeni” lilimaanisha “kuendelea kulinda amani”.
‘‘Baada
ya kutoa kauli hiyo kuna watu wakaeleza kuwa sasa Waziri Mkuu analeta
sera za kupiga. Hapana ilikuwa kujaribu kukemea watu wasilete fujo kama
kwamba Serikali iko likizo,’’ alisema Pinda.
Alisema
akiwa bungeni aliwahimiza Watanzania kuilinda amani na utulivu uliopo
nchini kwa gharama yeyote ile na iwapo atatokea mtu kutaka kuivunja
amani hiyo, hatapewa nafasi badala yake atashughukiwa kwa namna yeyote.
Waziri
Pinda alitoa kauli hiyo tata mwaka jana wakati wa kipindi
alichokianzisha bungeni cha mswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu,
baada ya kluulizwa kuhusu vitendo vya polisi kupiga rais badala ya
kuwafikisha mahakamani.
Kauli yake ilisababisha
wanaharakati kumjia juu na wengine kutaka kwenda mahakamani kutokana na
kwenda kinyume na misingi ya utawala bora.
Waziri Pinda alitoa tafsiri ya neno hilo alipoongea na wananchi
wa Mkoa wa Katavi wakati akihitimisha ziara yake kwa kukutana na
wananchi wa Tarafa ya Kabungu, Kata ya Mpanda Ndogo wilayani Mpanda.
Alisema amani iliyopo hapa nchini ni ya miaka mingi iwapo wakitokea watu wanaotaka kuleta chokochoko, watashughulikiwa tu.
Akizungumzia
wakimbizi walioko mkoani Katavi ambao wanatarajiwa kupewa uraia,
alisema ni lazima mkoa ujiandae kuwapokea raia hao wapya na hiyo nayo ni
changamoto kubwa kwa mkoa.
‘‘Wakimbizi hao
wanaotarajiwa kupewa uraia ni wengi kwani ni zaidi ya 120 na changamoto
kubwa iliyo mbele ya mkoa. Hivyo ni vyema utaratibu mzuri ukaandaliwa
kwa ajili ya kuwapokea raia hao wapya na mkoa umejiandaa vizuri
utalifanyia kazi suala hilo kuhakikisha amani iliyopo inatunzwa,”
alisema.
Alisema mbali ya wakimbizi hao walioko makazi
ya Mishamo wapo wakimbizi wengine walioko kwenye makazi ya Katumba ambao
nao wanakaribia kufikia 80,000 ambao pia watapewa uraia.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment