

Na mbeyayetublog
Taarifa zilizotufikia muda huu ambazo Hazijathibitishwa Rasmi zinasema kwamba Basi la Dar Express lenye namba za usajili T 244 BXQ limekamatwa na Gunia zaidi ya 16 za Mirungi katika kituo cha ukaguzi cha Chekeri Korogwe Likitokea Arusha Basi Hilo lilikamatwa Jana Majira ya Saa nane Mchana na kupelekwa mpaka katika kituo cha wilaya cha Polisi Korogwe, mtu mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kuhisiwa anahusika na tukio hilo pia Konda wa Basi hilo anashikiriwa na Polisi.

Askari wa Jeshi la Polisi wakiwa wanapakia Magunia ya Mirungi katika Gari lao
Kwa
Taarifa ambazo Bado Hazijathibitishwa Rasmi zinasema kwamba kuna
Shehena kubwa ya Milipuko ya hatari inayotumika kutengenezea Mabomu ya
Kuvulia samaki na Kutengenezea Milipuko ya kupasulia Miamba Migumu
Imekamatwa Eneo la Korogwe Mchana Huu Wakati wa Jeshi la Polisi
walipokamata Basi la KLM EXP lenye usajili wa namba T491 ARB kwa ajili
ya Ukaguzi. Milipuko hiyo ambayo imesafirishwa kwa njia ambayo sio
sahihi kutokana na hatari yake ya kuwa kulikuwa na abiria na kama Basi
Lingetingishika zaidi Ingeweza Kulipuka .
Taarifa zaidi itakuja hapa.. fuatilia

Basi Hilo baada ya Kukamatwa

Milipuko hiyo baada ya kukamatwa mchana huu

Askari wa Jeshi la Polisi Katika Kituo cha Korogwe akikagua Milipuko hiyo
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment