MCHEZA
filamu za Kibongo Jennifer Kyaka ‘Odama’, amedai kuwa mwanaume ambaye
anaweza kumuoa jambo la kwanza lazima atambue kuwa yeye anafanya filamu
kwa muda mrefu hivyo hawezi kuacha kazi yake kwa sababu ya kuingia
kwenye ndoa.
Mcheza filamu za Kibongo Jennifer Kyaka ‘Odama’.
Odama alifungua kinywa chake baada ya kuzungumza na paparazi wetu,
ambapo alidai kuwa haiwezi kutokea kuacha kufanya filamu ili amridhishe
mwanaume kwani maisha yake yamekuwa yakiendeshwa na kazi hiyo kwa muda
mrefu.
“Naamini kuwa yule ambaye atakuja kwa nia ya kunioa kwanza lazima
atambue kuwa nafanya filamu, sitahitaji anieleze jambo la kuacha kazi
yangu, mimi ni mwanamke ambaye nahitaji kupata maendeleo kupitia kazi
zangu,” alisema.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment