MTANGAZAJI wa runinga Maimartha Jesse, ameweka wazi
kuwa pamoja na watu kulalamika kuwa mwaka uliopita ulikuwa mgumu kifedha
kwa upande wake amefanikisha kuingiza kiasi cha shilingi milioni 28
ambazo amezipata kupitia kazi zake za kila siku ikiwemo ya kundi lake
maarufu la Baikoko.
Mtangazaji wa runinga Maimartha Jesse.
Maimartha alifunguka mchongo huo wa kudaka kiasi hicho cha pesa baada
ya kuzungumza na mwandishi wetu, ambapo alisema kuwa huwa anafanya kazi
zake si kwa kumtazama mtu usoni na hiyo ndiyo sababu kubwa iliyomfanya
kuvuna kiasi hicho cha pesa.
“Nimepata pesa nyingi maana kama ningekaa tu nyumbani nisingeweza
kupata hata hizo milioni 28, namshukuru Mungu kwa sababu nimeweza
kufanya kazi zangu kwa ubora na kupata kiasi hicho, lakini kifupi ni
kwamba sijafanya dili feki za kupata pesa,” alisema Maimartha.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment