HOFU!
Waigizaji wa tasnia ya filamu Tanzania, ambao walikuwa wameanza
kusahausahau misiba mfululizo iliyowatokea miaka michache iliyopita,
juzikati walijikuta wakitoneshwa kidonda, baada ya kutokea kifo cha
muigizaji Tino Madhahabu, kilichotokea Tunduma mkoani Mbeya, kufuatia
kuugua kwa muda mrefu.
Muigizaji Tino Madhahabu enzi za uhai wake.
Msanii huyo aliyetamba katika uigizaji akiwa na Dude katika kipindi
maarufu cha Bongo Dar es Salaam, kwa muda wa miaka saba na baadaye
kuingia kwenye filamu alikuwa akiugua ugonjwa wa moyo, kiasi cha
kumfanya arejee nyumbani kwao kwa ajili ya matibabu, ambayo hata hivyo,
yameshindwa kunusuru uhai wake.
Wasanii kadhaa waliozungumza na Ijumaa
baada ya taarifa za msiba huo walionesha hofu ya kifo waliyonayo lakini
wengi wakasema Kifo cha Tino ni mipango ya Mungu hivyo kila mmoja
ajiandae tu.
Msanii aliyewahi kufanya kazi kwa karibu na Tino, Kulwa Kikumba ‘Dude’ alisema: “ Dah! Ni kweli jamaa katutoka, kikubwa tumuombee na hilo la hofu ni vyema kila mmoja akawa nayo ili aweze kujiandaa kwa safari.”
Msanii aliyewahi kufanya kazi kwa karibu na Tino, Kulwa Kikumba ‘Dude’ alisema: “ Dah! Ni kweli jamaa katutoka, kikubwa tumuombee na hilo la hofu ni vyema kila mmoja akawa nayo ili aweze kujiandaa kwa safari.”
Msanii wa filamu Bongo, Devota Mbaga.
Katika kuonesha kuweweseka, msanii mwingine wa filamu, Miriam Jolwa
‘Jini Kabula’ alisema: “Mimi sitakufa kwa kuwa niko karibu na Mungu,
watakaokufa ni wale walio mbali na Mungu.”Msanii mwingine, Isabela alisema kifo cha Tino kimemshtua mno na kusema ni mapenzi ya Mungu, lakini akaponda utabiri wa mchungaji akisema hajawahi kuamini mambo hayo, kauli ambayo pia ilitolewa na Rose Ndauka.
Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, kulikuwa hakuna taarifa rasmi zilizotolewa juu ya mazishi ya msanii huyo.Mungu Ilaze roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amina- Mhariri
Imeandikwa na Hamida Hassan, Gladness Mallya na Deogratius Mongela.
Msanii huyo aliwahi kuhojiwa na Global TV Online akizungumzia ugonjwa wake pamoja na kuomba msaada
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI
Post a Comment