Mateka hao ni Kenji Goto Jogo mwandisi wa habari
 aliyekuwa anaandika kuhusu vita vya ndani vya Syria mwaka jana, na  
Haruma Yukawa mwanajeshi kutoka kampuni binafsi aliyekamatwa nchini 
Syria mwezi Agosti mwaka jana.
Tishio  hilo limekuja baada ya Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe, 
kuahidi kutoa kiasi hichohicho cha fedha  kama msaada usiokuwa wa 
kijeshi kwa nchi zinazopigana dhidi ya ISIS.Video hiyo iliyosambazwa katika tovuti zinazohusiana na wapiganaji hao, ziliomwonyesha mpiganaji mwenye lafudhi ya Kiingereza ambaye anajulikana kama ‘Jihadi John’ aliyeonekana katika video za mauaji ya kuwakata vichwa mateka David Haines, Alan Henning (Waingereza), na James Foley na Steven Sotloff (Wamarekani) hivi karibuni.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI 
 
 
 
.jpg) 
 
 
 
 
Post a Comment