Habari za kuwepo kwa uhusiano mbaya kati ya nyota wa Barcelona, Lionel Messi na kocha wake Luis Enrique
 mpaka sasa sio mpya masikioni mwa mashabiki wa soka barani ulaya baada 
ya matukio kadhaa ambayo yamekuwa yakitokea ndani ya klabu hiyo ya Nou Camp.
Tetesi zaidi zinadai kuwa kocha Luis Enrique amepewa mechi mbili kuokoa kazi yake jambo ambalo Barcelona imekanusha laki ni hakuna asiyefahamu kuwa Messi na kocha wake hawaelewani.
Chanzo cha ugomvi baina ya wawili hao 
kimefahamika baada ya ripoti kadhaa toka kwa watu walioko karibu na 
klabu hiyo kufichua kuwa ugomvi huu ni mkubwa kuliko inavyodhaniwa na 
umefikia hatua mbaya.
Messi na Luis Enrique 
Ripoti tofauti zinasema kuwa Messi
 na kocha wake waligombana siku ya ijumaa wiki iliyopita na ugomvi 
ulikuwa mkubwa kiasi cha wawili hao kukunjana na kutaka kupigana kabla 
ya kuachanishwa na wachezaji wa Barcelona.
Messi ambaye alichelewa kujiunga na kambi ya Barcelona
 baada ya kutoka kwenye mapumziko nyumbani kwao Argentina aliingia 
mazoezini siku hiyo ya ijumaa na kuungana na wenzie ambao walikuwa 
wakifanya mazoezi ya kucheza mechi ya wenyewe kwa wenyewe huku Enrique akiwa refa.
Katika mazoezi hayo Messi alichezewa rafu ambayo alitaka kupewa adhabu ndogo lakini Enrique hakupuliza filimbi jambo ambalo lilimkera Messi na kumfanya aanze kumshutumu Enrique.
Baada ya mazoezi hayo kumalizika Messi alimfuata Enrique na kuanza kutupiana nae maneno mpaka kufikia kukunjana kabla Neymar hajaingilia ugomvi huo na kuwatenganisha kabla hawajapigana.
Kufuatia ugomvi huu Enrique alimuacha Messi benchi kwenye mchezo uliofuata dhidi ya Sociedad na nyota huyo alijibu mapigo kwa kutohudhuria mazoezi ya jumatatu.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI. 
Post a Comment