Chama cha mapinduzi CCM kimevitaka vyombo vinavyotakiwa kuchukuwa
hatua dhidi ya watuhumiwa wa sakata la Tegeta Escrow baada ya bunge
kumaliza jukumu lake vitimize wajibu wao kwa wakati kwa kuchukuwa hatua
stahiki kwani kadri vinavyochelewa vinasababisha maswali mengi kwa
wananchi.
Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Bw Nape Nnauye ameyasema hayo
jijini Dar es Salaam ambapo amesema wakati umefika sheria iangaliwe upya
viongozi wanapojiuzulu wasiwe wanawajibika kisiasa tu bali wawajibike
pia kwa hasara waliyosababisha ili iwe fundisho kwa waliopo na vizazi
vijavyo na kuongeza kuwa mtu anapojiuzulu na kuisha hapo inampa furasa ya
kwenda kutumia alizochuma.
Akizungumzia suala la vurugu zinazoendelea nchini wakati wa
kuapisha wenyeviti na wajumbe wa serikali za mitaa Bw Nape amesema chama
chake kinalaani vurugu hizo na kuwataka wasioridhishwa na matokeo ya
uchaguzi huo kufuata taratibu kwani vurugu hizo wakati mwingine zimekuwa
zikisababisha watu kuumia.
Post a Comment