Staa Afrika Mashariki, Nasibu Abdul ‘Diamond’,
amefunguka kwamba haamini kama kweli amepata nafasi ya kutumbuiza kwenye
sherehe za utoaji tuzo za wanamichezo bora zilizoandaliwa na Shirikisho
la Soka Afrika (CAF) ambazo zimefanyika usiku wa kuamkia leo jijini,
Lagos, Nigeria.
Akizungumza na Mpekuzi, Diamond amesema amefurahi kupata nafasi ya
pekee ambayo mara nyingi hutolewa kwa wasanii wakubwa Marekani na
kuamini kwamba muziki wa Tanzania unathaminika kila kona.
“Nimefurahi maana hii inaonyesha jinsi gani muziki wetu umekuwa hadi
kufikia Afrika kuwa moja ya kionjo hasa kwenye tamasha kubwa kama hilo,
kiukweli sikuwahi kufikiria hapo mwanzo,” alisema Diamond.
Post a Comment