Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Aliyetoa Tuzo ya bidii ya kazi kwa Wanyama, aliwahi kuspend Valentine na mbuzi (Video hapa)



_80131238_109692361 
Mwanasiasa mmoja nchini India, ameweka historia ya aina yake baada ya kuwatunuku Tuzo ya uaminifu wanyama kadhaa ikiwemo punda na swala akisema wameonyesha uaminifu mkubwa na kuwazidi binadamu.
Vatal Nagaraj, ndiye mwanasiasa ambaye aetoa tuzo kwa wanyama hao baada ya kujiridhisha kuwa ni waaminifu na ni waaminifu, hutekeleza wajibu wao kwa nidhamu kubwa, huku wanyama wengine aliowatunuku ni pamoja na mbwa na ng’ombe.
Wakati wa utoaji wa tuzo hizo, wanyama hao walipendeza kwa kuvalia shanga.
Punda walionekana kuwafurahisha watazamaji waliokusanyika katika sherehe hiyo kwani walikuwa wamepambwa maua, mwanasiasa huyo amesema punda hutumiwa kwa kiasi kikubwa kufanya kazi nchini humo lakini jamii nyingi bado hazitambui mchango wao.
Love yake kwa wanyama haikuanza leo, mwaka jana aliwahi kuzungumziwa kwa kituko chake alichokifanya kwa kusherehekea siku ya Valentine akiwa na mbuzi!
Mcheki kwenye video hii.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright BONGO HABARI
Back To Top