Miezi michache tangu ahamishie makazi yake nchini Afrika Kusini, modo
aliyetikisa Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ ametia aibu kutokana na
kudaiwa ‘kujiuza’ kwa njia ya mtandao nchini humo.
Chanzo kilicho karibu na staa huyo kimedai kuwa, Masogange yupoyupo tu,
kazi kujipiga picha za utupu na kuzitupia mtandaoni kana kwamba
anatafuta wanaume.
“Kimsingi hana kazi huku Sauz zaidi ya kuposti picha kwenye mtandao wa
Instagram na anachanganya sana wanaume wenye pesa zao, si unajua tena
mtoto kajaliwa shepu la maana.
“Ukitaka kuthibitisha hilo ninalokwambia, ingia katika akaunti yake
utaona picha kibao za kihasara akiwa hotelini, kama siyo kutuaibisha na
kujiaibisha mwenyewe ni nini?” kilihoji chanzo hicho.
Baada ya chanzo hicho kuvujisha habari hiyo, mwandishi wetu aliingia
kwenye akaunti ya mrembo huyo na kujionea picha kibao zenye mapozi ya
kihasara.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI
Post a Comment