Hatua ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya ilimalizika usiku wa jumatano ikishuhudia michezo nane ambayo ilipigwa kwenye viwanja tofauti barani humo .
Katika michezo iliyopigwa siku hiyo Fc Barcelona walijihakikishia ushindi wa Kundi F baada ya kuwafunga mabingwa wa Ufaransa PSG kwa matokeo ya 3-0 .
PSG ndio walioanza kufunga kwenye mchezo huo kupitia kwa mshambuliaji wa Sweden Zlatan Ibrahimovic bao ambalo halikudumu kwa muda mrefu kwani Lionel Messi alisawazisha .
Kipa wa PSG akiruka bila mafanikio akijaribu kuokoa mpira uliopigwa na Neymar.
Kazi katika usiku mzuri kwenye uwanja wa Nou Camp ilimalizwa na mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez aliyefunga bao la tatu .
Matokeo haya yanawafanya Barcelona kufuzu kama washindi wa kundi lao huku PSG nao wakifuzu kama washindi wa pili.
Kwingineko Manchester City wakiwa ugenini kwenye mji mkuu wa Italia walifanikiwa kuwafunga As Roma 2-0 ushindi ambao umewapa tiketi ya kufuzu hatua ya 16 bora kama washindi wa pili kwenye kundi lao nyuma ya Bayern Munich.
City walifunga kupitia kwa Samir Nasri na Pablo Zabaleta ushindi uliowafanya wafikishe pointi nane .
Samir Nasri akishangilia na wenzie baada ya kuifungia Manchester City bao la kwanza katika ushindi wa 2-0 dhidi ya As Roma.
Wachezaji wa Chelsea wakishangilia moja kati ya mabao matatu waliyofunga dhidi ya Sporting Lisbon .
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment