Ni
wiki nyingine tulivu kabisa tunakutana kupitia safu hii nikiamini
umzima na unaendelea nyema na maandalizi ya sikukuu za Christmas na
Mwaka Mpya.Mimi
namshukuru Mungu kwa kila jambo ambalo amekuwa akinitendea katika kila
siku ya maisha yangu na nimuombe tu anijaalie niwe miongoni mwa wale
watakaouona mwaka 2015 wakiwa wazima.
Mpenzi msomaji wangu, kilio cha wengi
walio kwenye uhusiano ni kusalitiwa na wapenzi wao waliotokea kuwaamini
sana. Wapo ambao si tu kwamba wanahisi bali wanawafumania kila kukicha
waume/wake zao licha ya imani waliyokuwa nayo kuwa hawawezi kusalitiwa.
Imefika wakati baadhi yetu hatutaki hata
kufuatilia nyendo za wenza wetu tukijua kwamba kufanya hivyo ni
kujitafutia presha za bure. Labda mimi naweza kuwa na uelewa tofauti
katika hili la kufuatilia nyendo za wapenzi wetu. Ninachojua mimi ni
kwamba, ili uwe na amani moyoni mwako juu ya mwenza wako lazima
uthibitishe kama kweli anakupenda na ametulia.
Utafanya hivyo kwa kufuatilia nyendo
zake bila yeye kujua na katika kufuatilia kwako ndipo utajua kama kweli
umempata mwenza sahihi ama laa. Wapo ambao husimamia kwenye ule msemo
kwamba, ukimchunguza sana bata humli! Jamani ule ni msemo tu, tunajua
kila mmoja ana mapungufu yake ila ni vyema ukayajua ya wako ili ujue
namna sahihi ya kuishi naye.
Nalazimika kusema haya kwa kuwa, kasi ya
wapenzi kusalitiana imekuwa ikishika kasi kila siku kiasi cha baadhi
kuhisi bila kusaliti hawasikii raha. Yaani wanapatilizwa kila kitu na
wenza wao lakini bado wanatoka nje.
Unakuta mwanaume ana mke mzuri anayejua
mapenzi na kila kitu lakini bado mwanaume huyo haridhiki. Pia wapo
wanawake ambao wamebahatika kuwapata wanaume ‘handsome’, wanaojua
mapenzi na kujali pia lakini bado tamaa za usaliti wanakuwa nazo.
Ukiuliza kipi kigeni wanachofuata huko nje, jibu hakuna.
Watu wa sampuli hii ni vyema kuwabaini
kuliko kubaki na ile imani kwamba, anakupenda na hawezi kukusaliti. Una
ushahidi gani kama kweli anakupenda na hakusaliti huko anakopita?
Hivi leo ukiambiwa utaje sababu inayokufanya uamini kuwa mwenza wako hachepuki utatoa sababu gani? Hakika huwezi kuwa nayo, sanasana utaishia kusema unamuamini kwa kuwa hujawahi kumfumania wala kuona dalili za kuzungukwa.

Kizuri ni kwamba, ukifuatilia sana
utagundua wengi wetu hutuna imani ya asilimia 100 ya kutosalitiwa. Wengi
wetu licha ya wenza wetu kuonyesha wametulia, bado hatuwaamini
kupitiliza. Hii yote ni kwa sababu akiamua kukusaliti anaweza kufanya
hivyo na wewe usijue lolote.
Nilishawahi kufanya uchunguzi huko nyuma
kwa kuzungumza na baadhi ya watu kuhusu hili suala la kusalitiwa. Wengi
walikiri kujua kwamba wanasalitiwa lakini wenyewe wanadai ni mambo
ambayo wakiyafuatilia hawawezi kudumu kwenye ndoa zao.
Ni kweli niliobahatika kuongea nao
kwenye hili ni wachache sana lakini maelezo yao yamenifanya niwe na
uhakika wa hiki ninachokiandika leo.
Kipi kifanyike?
Kutokana na maelezo yangu hapo juu utakubaliana na mimi kwamba hakuna anayeweza kusimama mbele za watu na kuthibitisha kuwa hasalitiwi. Kikubwa ni wewe na mimi kuwaamini wapenzi wetu.
Lakini pia hakuna ubaya kama utafuatilia na kujua kama kweli uliye naye ametulia na hachepuki. Usibaki kuamini kibubusa kwamba husalitiwi, wakati mwingine fuatilia nyendo zake bila yeye kujua.

Najua kweli ukifanya hivyo unaweza
kugundua madudu mengi kwa huyo uliyenaye na ukajikuta unachanganyikiwa
lakini ni bora utakuwa umejua yaliyojificha ili uchague mwenyewe kusuka
au kunyoa.
Heri ujue kisha kama huwezi kumuacha, uzungumze naye, abadilike kuliko umuache aendelee kufanya ufuska wake gizani kisha wewe ubaki na imani kwamba ametulia na hawezi kukusaliti.
Heri ujue kisha kama huwezi kumuacha, uzungumze naye, abadilike kuliko umuache aendelee kufanya ufuska wake gizani kisha wewe ubaki na imani kwamba ametulia na hawezi kukusaliti.
Lakini kama moyo wako unagoma
kumfuatilia mpenzi wako na moyo wenyewe unakuhakikishia kwamba mwenza
wako katulia, basi baki na imani yako hiyo.Lakini kwa ulimwengu wa sasa
kama utakuwa umejihakikishia kwa asilimia 100 kwamba una mpenzi ambaye
hajawahi kukusaliti na wala hafikirii, jiweke kwenye kundi la watu
waliobahatika na Mungu awabariki sana.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment