Mwanamke mmoja ambaye jinalake ni Rahma,
kutoka Cairo, Misri, amedai talaka kwa mumewe kwa kuwa amekuwa si
mwaminifu, amekuwa akimsaliti mara kwa mara kutokana na kile ambacho
mwanamke huyo amekisema eti mumewe anataka mke wake afanane na Kim Kadarshian au muigizaji Haifa Wehbe.
Mara kadhaa mume wa mwanamke huyo
amekuwa akimtaka avae na kutengeneza nywele zake ili afananena mmoja ya
mastaa hao, alikataa, amesema anatazama mambo mengine ya msingi
kuyafanya ikiwemo kumlea mtoto wake wa mwaka mmoja, hivyo asingeweza na
hili la kujitengeneza ili afanane na mastaa hao ambao yeye aliwaita
midoli wa kwenye TV!
Kwa kuwa dini ya mwanamke huyo inaongozwa na Sheria ya Shariah
ambayo inaruhusu mwanamke kuachika na mahari iliyotolewa kurudishwa,
mwanamke alifanya maombi ya kudai talaka ili aendelee na maisha yake
mengine.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment