Raphael Tenthani
Katika
maisha ya kawaida tumezoea kuona kuwa watangazaji na waandishi wa
habari hupendelea kuonekana SMART kwani wao ni kioo cha jamii,,ila kwa
hili ni tofauti
Aina
yake ya mavazi na uvaaji wake umezua gumzo katika mitandao jamii. Ralph
amezoeleka kuonekana katika mavazi ya 'hovyo hovyo', yaliyolowa,
machakavu na yaliyotoboka huku viatu vikiwa vimeachama, nywele 'vululu
vululu' na sura ya 'kilevi'.
Mwandishi
huyu wa habari hujihudhurisha alivyo katika kazi zake mbalimbali za
kuhojiana na kurusha habari bila kujali ustaarabu wa eneo husika hata
ikiwa ni kwenye zulia jekundu.
Wengi
wanasema mkosoaji huyu mkubwa wa Serikalizote zilizoongozwa na Marais
ndugu, Bingu (marehemu) na Peter Mutharika, huenda anafanya hivyo ili
kutimiza masharti ya 'mganga' aliyemsaidia kupata ujasiri,akili nyingi
na kazi katika shirika kubwa la utangazaji la BBC. Wanadai ikiwa
atakiuka masharti hayo, huenda akapoteza kazi yake na kuwa 'juha'.
Vyovyote viwavyo, Raphael "Ralph" Tenthani bado ni mwakilishi wa BBC nchini
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment