WASANII wengi wa kike wamekuwa na tabia ya kuibiana mabwana jambo ambalo wenyewe wamekiri kwamba wako kwenye hatari ya kupukutika kama kuku kwa ugonjwa hatari wa Ukimwi.Wakizungumza na Ijumaa hivi karibuni, baadhi ya mastaa wenye majina makubwa Bongo walifungukia kamchezo hako ka kushea mabwana na wakati mwingine hufanya tendo hilo pasipo kutumia kinga.
Tujiunge na baadhi ya mastaa waliozungumzia ishu hiyo:
Staa katika tasnia ya filamu Bongo,Tamrina Poshi 'Amanda'.
TAMRINA POSHI ‘AMANDA’Wasanii wa kike wengi ni malimbukeni kwani wakiona flani ana maendeleo na yupo na mwanaume flani wanammendea na kumchukua. Nina uhakika kutokana na tabia hii wengi tukienda kupima Ukimwi itakuwa ni hatari, hakuna atakayepona.
TIKO HASSAN
Tabia hii ni ushamba pia kutokuwa waaminifu. Wapo wasanii walishawahi kunichukulia mwanaume wangu lakini siwezi kuwataja ila inakera sana.
Kama ni ugonjwa wa Ukimwi basi utatuua wengi kwa sababu ya ushamba maana mtu akikuona uko na mtu wako anammendea wakati kabla hujawa naye walikuwa wanapishana tu.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo,Zuwena Mohamed 'Shilole'.
ZUWENA MOHAMED ‘SHILOLE’Ukweli hawana adabu na hawajafunzwa huko makwao. Kutokana na tabia hii ya kuchukuliana mabwana wengi tutaambukizana Ukimwi maana hatujiheshimu.
ISABELA MPANDA
Mimi nasema hivi, asilimia 90 ya wasanii wa kike wana Ukimwi kwa sababu wana tamaa sana. Utakuta mwanaume mmoja anatoka kimapenzi na wasanii kumi huoni hii ni hatari?
ISABELA FRANCIS ‘VAI WA UKWELI’
Huwa nawasikia mastaa wengi wa kike wakilalamika kuibiana mabwana lakini mimi sijawahi kuiba nimetulia na Bonny wangu. Lakini tukija kwenye suala la maradhi ukweli kwa tabia hiyo, ni rahisi sana kuambukizana Ukimwi.
SALOME URASSA ‘Thea’
Tuache hiyo tabia ya kujirahisisha kwa sababu kwanza wanaume wanatudharau pia jamii inatuona sisi wasanii ni m****** ukiona mwenzako ana mtu wake mheshimu kama shemeji yako.
Kwa staili hii, Ukimwi ukianza kuua, itakuwa ni hatari kwa sababu asilimia 80 tutakufa kwa ngoma.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Lulu Semagongo 'Aunt lulu.
LULU SEMAGONGO ‘AUNTY LULU’Hii tabia ya kuibiana mabwana ipo sana kwani unakuta mtu anajua kabisa mimi natoka na mwanaume flani naye anajipenyeza. Ukimwi utatumaliza kila siku maana mzunguko wa wanaume na wanawake ni uleule.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment