Vunja ukimya! Kwa mara ya kwanza, mama mzazi wa mwanamitindo na mkurugenzi wa brand ya urembo ya Kidoti, Jokate Mwegelo, Benadertha Ndunguru amemfungukia mwanaye baada ya kuingia ubia na Kampuni ya Rainbow Shell Craft ya nchini China inayomuingizia mabilioni ya fedha.
Mkurugenzi wa brand ya urembo ya Kidoti, Jokate Mwegelo akifurahia jambo na mama yake mzazi, Benadertha Ndunguru.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda mara baada ya mwanaye kusaini mkataba
huo kwenye Hoteli ya Serena, Dar, mwishoni mwa wiki iliyopita, mzazi
huyo alimmwagia Jokate sifa tele na namna anavyofurahishwa na maendeleo
yake.
Jokate Mwegelo akilamba dili nono kutoka kwa wachina.
“Jokate ni mwanangu wa tatu kuzaliwa. Najivunia akili yake, uwezo
wake, namna anavyojituma, namshukuru sana Mungu kwani anafanya mambo
makubwa kulingana na nafasi yake,” alisema mama Jokate.
Jokate Mwegelo akipiga picha na mwakilishi wa kampuni ya Rainbow Shell Craft ya nchini China.
Kwa upande wake, Jokate aliliambia Ijumaa Wikienda kwamba
amefurahishwa na ubia huo kwani mbali na masuala ya urembo pia kupitia
brand yake anatarajia kuongeza ajira kwa akina mama kwani kitajengwa
kiwanda ambacho kitatoa ajira kwao.
Jokate Mwegelo na mama yake mzazi wakipata picha ya ukumbusho na wadau wengine.
“Hii ni fursa kubwa kwetu Tanzania, nawashukuru sana vijana wenzangu
ambao tulikaa na kubuni brand ya Kidoti, leo imenipa heshima kwa
Watanzania na inakuja kutufaidisha,” alisema Jokate.Kwenye hafla hiyo fupi ambayo staa huyo alilamba Sh. Bilioni 8.5, wageni rasmi walikuwa ni Mheshimiwa Mariam Msangi, Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) ambaye pia ni mama mdogo wa Jokate na Mstahiki Meya wa Ilala, Jerry Silaa ambao walimpongeza kwa hatua hiyo.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment