Peter Kassig enzi za uhai wake.
Kanda moja ya video iliowekwa mtandaoni inaonyesha mauaji ya mtu wa
kutoa huduma za misaada raia wa Marekani Abdul Rahman Kassig ambaye
alikuwa anajulikana kama Peter Kassig kabla ya kutekwa nyara na
wanamgambo wa Islamic State nchini Syria mwaka uliopitaVideo hiyo
inamuonyesha mwanaume mmoja anayeonekana kuwa mwanachama wa Islamic
State akiwa na kisu mkononi na maandishi yanayosema kuwa Peter Kassig
ameuawa.
Peter Kassig mda mchache kabla ya kukatwa shingo na wapiganaji wa IS
Kanda hiyo pia ina picha za watu kadha waliouawa ambao wanasemekana
kuwa wanajeshi wa Syria waliokuwa wametekwa nyara.Marekani imesema kuwa
inafanya juhudi za kubaini chimbuko la kanda hiyo.
Bwana Kassig ambaye anajulikana kama Peter alitekwa nyara mwaka
uliopita.Mnamo mwezi Octoba kanda nyengine ya video ya kifo cha
mfanyikazi mwengine wa misaada kutoka Uingereza Alan Henning iliisha
huku Kassig akitishiwa.
(Chanzo: BBC)
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment