DEREVA
wa bodaboda aliyefahamika kwa jina moja la Fikiri, nusura amuue mrembo
mmoja mkazi wa Tandale-Kwatumbo, jijini Dar baada ya kumparamia na
bodaboda kando ya barabara.
Mrembo
(jina halikufahamika mara moja) aliyenusurika kifo baada ya kugongwa na
mwendesha bodaboda aliyefahamika kwa jina moja la Fikiri.
Katika tukio hilo lililotokea hivi
karibuni, dereva huyo wa bodaboda akiwa anatokea upande wa Kwamtogole
kuelekea Magomeni-Makanya, alipokaribia kona ya kuelekea Magomeni-Kagera
ndipo akamvaa mwanamke huyo aliyekuwa akijipitia zake na kumfanya
apoteze fahamu kwa dakika kadhaa.
Raia wakishuhudia ajali iliyotokea.
Chanzo kimeeleza kuwa, mwendesha bodaboda huyo alikuwa kasi
‘akamu-overtake’ mwenzake lakini baada ya kuchomoza mbele yake alikutana
na bodaboda nyingine ambayo alivaana nayo na kwenda kumkumba mrembo
huyo, akaanguka na kuzimia.
Bodaboda huyo na abiria wake mwenye asili
ya kiarabu walitumbukia kwenye mtaro na kugalagala kwa dakika kadhaa
kabla ya kuchomolewa na wasamaria wema.
Bodaboda ikiwa mtaroni baada ya ajali.
Baadaye mrembo huyo alizinduka na kusema kuwa mwendesha bodaboda huyo
alimfanyia kitu mbaya sana kwa kuwa yeye alikuwa kando kabisa ya
barabara lakini alishangaa bodoboda hiyo kumfuata alipo.
Post a Comment