Kigogo wa taasisi moja ya mikopo (Saccos) wilayani Bagamoyo, Pwani, Shabani Rajabu Mkali akiwa na mke wa mtu gesti.
Tukio hilo la aina yake lilijiri kwenye gesti moja (jina tunalo)
iliyopo Kimara- Mwisho jijini Dar es Salaam ambapo mzee huyo alifika kwa
nia ya dhati ya kukutana na mrembo huyo aliyetambulika kwa jina la
Rehema, anayedaiwa kuwa ni mwalimu wa shule moja ya msingi mjini
Bagamoyo.Inadaiwa kuwa Rehema alikuwa akikutana na mzee huyo kwenye ofisi yake ya mikopo akitarajia kukopa fedha ili afanye biashara.
MTOA HABARI
Akizungumza na Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ya Global Publishers, mtoa habari wetu alisema mume wa mwanamke huyo, Matokeo Issa alikuwa na habari za mkewe kwenda kukutana na mzee huyo gesti, ndipo na yeye akafuatilia kwa nyuma ili kwenda kuwanasa.
“Wengine wanasema mume na mke walipanga kumnasa mzee huyo kwa vile alikuwa akimsumbua mara kwa mara, mke akamwambia mumewe.“Lakini wengine wanasema si kweli, mke alikwenda kwa kujificha lakini akaonekana na shemeji yake ambaye alimfuatilia kwa nyuma, alipoingia gesti akamwita kaka yake ndiyo wakamnasa,” kilisema chanzo hicho.
Kigogo Shabani Rajabu Mkali akiwa amesimama baada ya fumanizi.
Kikaendelea: “Lakini kwa taarifa zaidi mwoneni Mjumbe wa Serikali ya
Mtaa wa Kimara Bakery, anaitwa Tatu Kitambulio, yeye anajua kila kitu
maana baada ya mzee kunaswa aliitwa kuwa shahidi kwa vile ni mtu wa
serikali.”OFM YAMSAKA MJUMBE KITAMBULILO
Ili kupata ukweli wa madai hayo, OFM walimtafuta Mjumbe Kitambulio ambaye alikuwa na haya ya kusema:“Ni kweli, ilikuwa Agosti 24, mwaka huu, nilifuatwa nyumbani na kuambiwa kule gesti kuna mzee amekutwa na mke wa mtu.
“Nilitoka hapa hadi gesti, nikakuta tukio
lipo kweli. Mimi kama mjumbe ambaye nipo kwa niaba ya serikali, niliweka
sawa mambo kwamba badala ya kufikishana mbali, wakubaliane. Aliyekutwa
na mke wa mwenzake (mzee Mkali) akakubali kwamba atatoa shilingi milioni
tatu ili mambo yaishe.
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Kimara Bakery, Tatu Kitambulio akionesha picha ya kigogo akiwa na mke wa mtu .
“Ili kuweka ushahidi sawa alikubali kuweka ahadi yake kwenye
maandishi. Aliandika anakubali kukutwa na mke wa Matokeo Issa na kwamba
atalipa hizo pesa Agosti 26, mwaka huu kwa kumkabidhi mwenye mke.“Basi, ilipofika Agosti 26, tukampigia simu kumuulizia, cha ajabu akasema kama mume anataka hizo pesa azifuate Bagamoyo lakini ajue kwamba analipwa na mke anabaki kwake yeye huyo mzee, tukashangaa sana.
“Tena mbaya zaidi aliacha maandishi yake kwangu kama mjumbe na mashahidi wawili, Waliondo Ali na Nasoro Abeid,” alisema mjumbe huyo.
OFM WAMSAKA MUME
Baada ya kuzungumza na mjumbe, OFM walimpata mume wa mwanamke huyo ambaye alisema:
“Nilikuwa nikimfuatilia mke wangu hatua kwa hatua baada ya kugundua kuwa ana nyendo zisizokubalika na yule mzee (Mkali). Kwanza mzee amekuwa akimwekea bili ya vitu mbalimbali mke wangu na kumpa fedha za matumizi kama kilainisho.
Waraka ukionesha Mkali 'akijikomiti' kwa maandishi kulipa faini kama fidia baada ya kunaswa.
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Kimara Bakery, anaitwa Tatu KitambulioHata kama mke wangu alitaka mkopo iweje malipo yawe ngono?“Kabla ya sakata hilo, nilianza kushangaa kuona mke wangu anakuwa bize tofauti na kipindi cha nyuma ndipo nikambana na akamtaja yule mzee.
“Za mwizi ni arobaini siku ikafika, mzee akampigia simu mke wangu ili wakutane gesti huku akijua kufanya hivyo na mke wangu Rehema ni kosa kisheria.“Siku ya tukio mzee alitoka Bagamoyo anapoishi na kutimba Dar, akampigia simu, mimi nikajua na kumfuatilia mke wangu mpaka walipokuwa gesti na mimi nikaibuka na kuwanasa.”
INAVYODAIWA
Habari zinadai kuwa, mume alipowanasa wawili hao, mzee aliulizwa maswali yafuatayo:
Swali: Unafanya nini na huyu dada humu gesti?
Jibu: Nimekuja kumfundisha tuliyojifunza kwenye semina.
Swali: Unamfundisha kama nani yako?
Jibu: Nachukulia kama mwanangu nilikuja kumsaidia mizigo yake ili nitangulie nayo Bagamoyo.
Swali: Kwa nini unamwekea bili na kumpa fedha za matumizi?
Jibu: Mwanangu usinifanyie ukatili wowote mie nitalipa faini mtakayosema.
Swali: Utalipa shilingi ngapi kama faini?
Jibu: Semeni wenyewe.
Swali: Nataka utoe shilingi milioni tatu kama gharama nilizotumia kumsomesha mke wangu.
Jibu: Sawa, hakuna tatizo nitalipa baada ya siku tatu kuanzia leo mpaka kufikia tarehe 26, mwezi wa nane nitazileta kwa mjumbe.
MZEE MWENYEWE SASA
Baada ya kuzungumza na wote, OFM walimpigia simu mzee Mkali. Hali ikawa hivi:
OFM: Habari yako mzee? Shikamoo.
Mzee: Nani mwenzangu? Sema shida yako, nina mambo mengi.
OFM: Unamjua Rehema? Inadaiwa ulikutwa naye gesti pale Kimara Mwisho.
Mzee: Nasema uje mara moja huku Bagamoyo, vinginevyo nakuroga kijana.
Akakata simu.
Post a Comment