Nyota wa mchezo, Angel di Maria akiifungia Argentina bao la nne.
Di Maria akitoa pasi ya bao kwa Aguero (hayupo pichani).
Erik Lamela akiifungia Argentina bao la pili.
Federico Fernandez akipachika bao la tatu kwa Argentina dhidi ya Ujerumani.
Mario Gotze akiipatia Ujerumani bao la pili.
TIMU ya Taifa ya Argentina imelipa kisasi cha kufungwa bao 1-0 na
timu ya Ujerumani katika fainali za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil
kwa kuiporomoshea kipigo cha mabao 4-2.Argentina imetoa kichapo hicho katika mechi ya kirafiki iliyopigwa jana usiku katika Uwanja wa Esprit, Dusseldorf nchini Ujerumani ikiwa ni baada ya siku 52 tangu ifungwe na Ujerumani katika fainali za Kombe la Dunia 2014.
Katika mechi hiyo, mabao ya Argentina yaliwekwa kimiani na Aguero 20, Lamela 40, Federico Fernandez 47, Di Maria 50 huku ya Ujerumani yakifungwa na Schurrle 52, Gotze 78.
ViKOSI VILIKUWA HIVI:
UJERUMANI: Neuer (Weidenfeller 46), Durm, Howedes (Rudiger 77), Ginter, Grosskreutz, Kroos (Rudy 71), Kramer, Schurrle (Muller 57), Reus, Draxler (Podolski 33), Gomez (Gotze 57).
Waliokuwa benchi bila kutumika: Zieler, Hummels, Boateng.
ARGENTINA: Romero (Andujar 79), Rojo Federico Fernandez, Demichelis, Zabaleta (Campagnaro 77), Mascherano, Biglia, Perez (Augusto Fernandez 46), Di Maria (Alvarez 86), Lamela (Gago 68), Aguero (Gaitan 83).
Waliokuwa benchi bila kutumika: Higuain, Lavezzi, Basanta.
Mwamuzi: Bjorn Kuipers (Uholanzi).
Post a Comment