Kwa Sarika maisha ya umaskini ambayo Timothy anaishi sio kikwazo hata kidogo bali kwake hapo ndipo anapata raha na mapenzi ambayo anasema yamemridhisha na kumtuliza nyumbani kwa kijana Timothy.
Timothy alikuwa anafanya
kazi nyumbani kwa kina Sarika kama mjakazi lakini akafutwa kazi na baba
ya Sarika baada ya kupendana na msichana wake.Kwa sasa yeye ni tarishi
katika ofisi hii ya jimbo.Sarika hana kazi
Wawili
hao sasa wapo katika pilka pilka za kuanza maisha mapya ila kwa
pingamizi kali . Sarika Patel anasema kulingana na mila yao si sawa
kuolewa na mtu asiyekubaliwa au kuchaguliwa na wawazi wako. Wachumba kwa
kawaida hutoka jamii sawa.
Mbali
na tofauti ya rangi zao za ngozi , Sarika anatoka katika familia tajiri
kinyume na mumewe Timothy ambaye ni mlalahoi. Licha ya tofauti hiyo,
Sarika anasema wazazi wake hawangeweza kumzuia kumpenda amtakaye
Post a Comment