DEREVA
wa Basi la Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam (UDA) ambaye hakuweza
kufahamika jina lake mara moja, amejikuta akipewa kibano hevi na askari
wa usalama barabarani ‘trafiki’ baada ya kuleta ubabe wakati alipotakiwa
kutii sheria bila shuruti.
Askari wa usalama barabarani ‘trafiki’ wakimdhibiti dereva wa basi la Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam (UDA) aliyevunja sheria ya usalama barabarani.
Tukio hilo la aina yake lililosababisha usumbufu kwa abiria wa basi
hilo, lilitokea juzi Bamaga-Mwenge jijini Dar kufuatia dereva huyo
kukataa kuegesha pembeni basi hilo lenye namba za usajili T 619 CVP
lililokuwa limevunja sheria ya usalama barabarani.
Dereva huyo akionyesha ubishi wa kutotii maagizo ya 'trafiki'.
Imedaiwa kuwa, basi hilo lilishusha abiria
kinyume na sheria kwenye kituo kisicho rasmi maeneo ya Chuo cha Ustawi
wa Jamii, Kijitonyama, Barabara ya Shekilango.
Chanzo makini kilichoshuhudia tukio hilo
kimedai kuwa, kufuatia hali hiyo ndipo trafiki hao watatu walio makini
na kazi yao, walilisimamisha basi hilo ili kumsomea mashitaka dereva
huyo sambamba na kondakta wake lakini wakaleta ubishi na kutoa lugha
chafu kitendo ambacho trafiki hao walishindwa kukivumilia.
Askari wa usalama barabarani ‘trafiki’ wakimtoa nje dereva jeuri wa UDA.
“Waliendelea kutoa lugha chafu, hawakuonesha kutii amri ili waambiwe
walichokosea ndipo trafiki wakalazimika kuwadhibiti kwa kuwafunga pingu
baada ya kukataa kutii sheria bila shuruti, tunawapongeza trafiki hawa
kwa kuwataiti,” kilisema chanzo hicho.Baada ya trafiki kuwadhibiti wawili hao, mmoja wao alishika usukani, wenzake wakakaa kwenye viti na kuliendesha basi hilo hadi Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’ kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.
Wananchi wakishuhudia mkasa huo.
Siku za hivi karibuni kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya
wananchi kwamba, madereva wa mabasi ya Uda wamekuwa wakivunja sana
sheria kama wao wako juu ya sheria kuliko madereva wengine.Tunashauri madereva kuwa makini na watiifu pindi wanapokuwa barabarani ili kupunguza ajali ambazo nyingi kati ya hizo zimekuwa zikitokana na uzembe wa madereva kwa kutotii sheria za usalama barabarani-Mhariri.
Post a Comment